Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mahafali ya wanafunzi 400 waliosoma nje ya nchi yaiva
ElimuHabari

Mahafali ya wanafunzi 400 waliosoma nje ya nchi yaiva

Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya tatu ya wanafunzi waliosoma vyuo vikuu nje ya nchi yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Hayo yamesemwa leo tarehe 18 Agosti, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wakala wa vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link (GEL), Abdlulmalik Mollel wakati akizungumzia mahafali hayo.

Amesema mahafali hayo ya wanafunzi waliobahatika kusoma nje ya nchi na kuhitimu yatakayofanyika Jumapili tarehe 21 Agosti, 2022, yatafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi.

Amesema mabalozi wa nchi mbalimbali ambazo vijana hao wamesoma wamethibitisha kushiriki katika mahafali hayo.

Amesema kwenye mahafali hayo wamealika Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu Zanzibar na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU).

Amesema wengine waliothibitisha kushiriki ni Bodi ya Tiba Tanganyika (MCT), Bodi ya Uhasibu (NBAA), Sekretarieti ya Ajira ambayo ilikuwa ikitoa mafunzo kwa wahitimu kuhusu namna ya kujiajiri wanapomaliza masomo badala ya kusubiri kuajiriwa.

“Ili mahafali haya yafane mlengwa mkubwa ni mzazi na mtoto wake  kwa sababu mwanafunzi aliyesoma nje anakuja kusherehekea na wazazi na walezi waliojinyima kumlipia ada hivyo wanafunzi wametibitisha kushiriki,” amesema

Mollel amesema wanafunzi wanaotarajia kwenda nje ya nchi kusoma wataalikwa ili waweze kujifunza kutimiza malengo yao kama wenzao walioenda kusoma wakahitimu na wakarudi nyumbani kuleta ujuzi kusaidia maendeleo ya nchi yao.

Amesema wanafunzi wa Kitanzania watakaokwenda nje ya nchi watabebeshwa malengo ya kuitangaza nchi ili kusaidia jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akiitangaza nchi kwenye maeneo mbalimbali duniani.

“Tunamwona mama yetu anavyokwenda nje ya nchi yetu kuisemea katika rasilimali tulizonazo, fursa na uzuri wanchi yetu sasa peke yake hataweza tunataka watanzania watakaokwenda nje sasa hivi kuitangaza nchi liwe ajenda ya kipaumbele,” amesema Mollel

Amesema anataka kuona mwanafunzi anayekwenda nje ya nchi anaporudi anarudi na wawekezaji kwenye nyanja mbalimbali kama elimu na utalii badala ya kuhitimu na kurejea nchini wakiwa na vyeti vitupu.

 “Tunataka kuona kupitia wao tunapata watalii na wawekezaji wa elimu kwasababu hatuhitimu na vyeti tu tunapaswa kuhitimu na maarifa ili nchi iweze kupiga hatua,” amesema.

Amesema mahafali hayo ni kwa wanafunzi wote waliosoma nje ya nchi na siyo  tu kwa waliopitia Global Education Link hivyo aliwataka ambao hawakupitia GEL waingie kwenye tovuti ya GEL watakuta sehemu ya mahafali ili wajaze maelezo yao.

Amesema mwanafunzi anayeruhusiwa kushiriki kwenye mahafali hayo ni yule aliyehitimu  na anauthibitisho wa kuhitimu na uthibitisho ni cheti.

Amesema kuhitimu au kushindwa kuhitimu nje ya nchi kunategemea uwajibikaji wa mwanafunzi anapokuwa nje ya nchi hana usimamizi wa wazazi na walezi au taarifa potofu walizopata kuhusu vyuo wanavyoenda kusoma.

Mollel amesema kuna wanafunzi wanaenda kusoma nje ya nchi kwa kuchagua vyuo kwenye mitandao na wanapogundua kwamba havitambuliki wanaamua kuahirisha masomo.

 “Kuna changamoto ya ada, mwanafunzi anasoma chuo ambacho kinalazimisha ada ilipwe yote kwa wakati mmoja na mzazi anakwama kulipa na anazuiwa kuendelea lakini kupitia GEL lazima ahitimu kwanza mambo mengine yafanyike baadae,” amesema

Amesema kuna mambo mengi yanayosababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuhitimu nje ya nchi ikiwemo kujiingiza kweye mambo yasiyohusiana na masomo kutokana na kukosa usimamizi sahihi anapokuwa anaendelea na  masomo.

Amesema mahafali hayo ni kama daraja kwa wanafunzi hao kukutana na wawekezaji mbalimbali ili kama kuna fursa za ajira waweze kuchukua vijana hao ambao alisema wamehitimu kwa ufaulu mzuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!