November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahaba ya Zari kwa Mondi usipime

Spread the love

 

UKWELI ni kwamba penzi ni kama pembe la ng’ombe, kulificha huwezi! ndivyo mahaba ya Mwanamama Zarina Hassan kwa mkali wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz au Mondi’ yalivyojionesha wazi baada ya msanii huyo kutua nchini Afrika kusini. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Zari raia wa Uganda mwenye makazi yake huko Afrika Kusini, ni mzazi mwenza wa Diamond ambapo wawili hao wamefanikiwa kupata watoto wawili Princes Tiffa na Nillan pindi mapenzi yao yalipokuwa motomoto.

Licha ya kwamba mastaa hao sasa hawapo pamoja kimapenzi na Zari kuweka wazi kuwa sasa wanalea watoto pekee, mahaba kati ya wawili hao yamezidisha maswali kutokana na kile ambacho mwanamama huyo wa watoto watano anachokionesha kwa Mondi.

Tarehe 13 Novemba mwaka huu Zari ameweka video na picha kadhaa kupitia ukurasa wake wa instagram na Facebook akiwa kwenye mtoko na familia yake yaani Mondi na watoto wao wawili.

Zari alionesha wazi kuenjoy mtoko huo licha ya kwamba ulikuwa ni kwa ajili ya watoto wao, ambapo mara zote kwenye video hizo alionyesha uso we furaha na tabasamu na kufurahia uwepo wa Diamond.

Muda wote wameonekana wakiwapa furaha watoto wao lakini kwa kinachoonekana ni kama wazazi pia wanakula goodtime kwenye mtoko ule.

Zari ameweka zaidi ya video 20, katika instagram story yake huku akiweka picha moja kwenye instagram yake akiwa na familia yake.

Aidha, baadhi ya mashabiki zao wameonesha kukubali ama kupenda uwepo wao kwa pamoja na hata wengine wakitamani warudiane kwani wanasema wanapendeza wakiwa pamoja.

Itakumbukwa mapema Februari mwaka 2018 Zari na Diamond waliachana huku tayari mwanamama huyo akiwa na watoto wawili wa Diamond Platnumz.

error: Content is protected !!