Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli atoa siri Tizeba, Lugola kukatwa
Habari za Siasa

Magufuli atoa siri Tizeba, Lugola kukatwa

Erick Shigongo Mbunge wa Buchosa (Ccm)
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Rais John Pombe Magufuli, ameeleza mchakato wa kuwapata wagombea ubunge wa Buchosa jijini Mwanza na Mwibara mkoani Mara ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Buchosa … (endelea)

Katika mchakato wa kura za maoni za CCM, Erick Shigongo na Dk. Charles Tizeba walifungana kwa kupata kura 354 jimbo la Buchosa.

Dk. Tizeba alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo.

Katika jimbo la Mwibara, waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Kangi Lugola naye alifungana na Charles Kajege kwa kura 173.

Rais Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM, ameweka wazi kuteuliwa kwa Shigongo na Kajenge wakati akijinadi kwa wananchi wa Bukokwa, Jimbo la Buchosa leo Jumanne tarehe 8 Septemba 2020.

Amesema, baada ya kura za maoni kufanyika na kupata kura sawa, uamuzi ulibaki kwa viongozi wa juu wa chama hicho kufanya uamuzi wao wa mwisho.

Rais Magufuli amesema, walipokaa katika vikao vya uteuzi, wakafuatilia kati ya wagombea, ni nani alikuwa mjumbe wa mkutano huo wa kura za maoni na kukuta ni Dk. Tizeba na Lugola.

“Tulipotoa kura moja ya Tizeba, Shigongo akaongoza na Tizeba akawa wa pili” na ndivyo hivyo “tulifanya jimbo la Mwibara,” amesema Rais Magufuli

Mgombea huyo wa urais, amewaomba wananchi hao kumchagua Shigongo awe mbunge wao na Dk. Tizeba atatumika serikalini katika nafasi zingine kwani zipo nyingi.

Awali, akizungumza katika mkutano huo, Dk. Tizeba aliwaomba wananchi wa Buchosa kumchagua Shigongo huku akisisitiza kuwa “wale wapambe wa Tizeba nione mnanuna nuna. Tizeba aliongoza miaka 10, sasa ni zamu ya Shigongo naye aongoze.”

Kwa upande wake, Shigongo amewaomba wananchi kumchagua Magufuli ili awe Rais, madiwani na yeye mwenyewe ili wakawatumikie wananchi.

Shigongo amemweleza Magufuli kwamba, wananchi wa hali ya chini wanamatumaini na CCM kuwatumikia ili waweze kufikia ndoto zao ikiwemo wanafunzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!