Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Dili’ la Membe, Lissu, Maalim Seif hadharani
Habari za SiasaTangulizi

‘Dili’ la Membe, Lissu, Maalim Seif hadharani

Spread the love

KAULI kwamba ‘tutashirikiana’ kati ya Chama cha ACT-Wazalendo na Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeanza kudhihiri kwa vitendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja … (endelea).

Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema amesema, tayari amesema visiwani Zanzibar, yeye, chama chake na wafuasi wao watampigia kura za urais Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo visiwani humo.

“Sisi tunamuunga mkono Maalim Seif na tutampigia kura,” amesema Lissu tarehe 7 Septemba 2020 akiwa kwenye mkutano wa kampeni za Chadema katika viwanja vya Demokrasia, Kibandamaiti, Zanzibar.

Mara kadhaa, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa; John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema; Zitto Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na viongozi wengine wa vyama hicho walieleza, kwamba mazungumzo ya ushirikiano kati ya vyama hivyo viwili yanaendelea.

Lissu amesema, kwa Zanzibar mgombea anayekubalika kwa wananchi ni Maalim Seif, na kwamba msimamo wa chama hicho ni kumuunga mgombea anayekubalika ili kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Lengo ni kuiangusha CCM, tunamuunga mkono Maalim Seif kwa kuwa ndiye anayekubalika. Na nyingi mumuunge mkono mgombea urais wa Tanzania anayekubalika,” Lissu alitoa kauli hiyo bila kutaja ni mgombea wa upinzani anayetaka aungwe mkono ili kuing’oa CCM.

Ingawa Lissu amempigia kampeni Maalim Seif, Chadema kimemsimamisha Said Issa Mohammed kuwa mgombea urais visiwani humo.

Bernard Membe-ACT-Wazalendo

Wakati Lissu akitoa kaui hiyo, Bernard Membe, mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesitisha kampeni zake za urais kwa siku nne sasa.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kwamba, Membe amesitisha kampeni zake kutokana na kutokea kwa mambo ambayo hayajawekwa hadharani.

Kwa mujibu wa Arodia Peter, msemaji wa ACT-Wazalendo akizungumza na chombo kimoja hapa nchini kuhusu kusitishwa kwa kampeni za Membe amesema “kuna mambo yanawekwa sawa kwanza.” Hata hivyo, hakufafanua zaidi.

Awali, wakati akitambulishwa kwa wanachama wa ACT-Wazalendo katika Ukumbi wa Mliman City, Membe alisema iwapo vyama vya upinzani vitakuwa na mgombea anayekubalika kwa wananchi zaidi yake, atamuunga mkono.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!