Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Kongwa wamtega Rais Magufuli
Habari za Siasa

Madiwani Kongwa wamtega Rais Magufuli

Mfano wa reli itakayotumika na treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro
Spread the love

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, limemuomba Rais John Magufuli kujenga reli ya treni ya abiria ya mwendo kasi kuanzia Dodoma mjini hadi mji mdogo wa Kibaigwa mkoani humo, anaandika Dany Tibason.

Madiwani hao wamesema ni bausara reli hiyo kufika Kibaigwa ambako kuna soko kubwa la mahindi badala ya kuishia Bwigiri wilayani Chamwino ili kurahisisha wafanyabiashara wa mahindi kusafirisha mizigo yao kwa urahisi.

Wakizungumza katika kikao cha Baraza hilo Madiwani hao walisema ujenzi wa reli hiyo hadi Kibaigwa utakuwa ni faraja kwa wananchi hususani wafanyabiashara wanaopeleka mazao katika soko la Kibaigwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, White Zuberi amesema soko la Kibaigwa lina wafanyabiashara wengi kutoka maeneo mbalimbali katika mkoa wa Dodoma na ambao wamekuwa wakipata shida kusafirisha mazao yao kuelekea katika soko hilo.

“Mheshimiwa Rais Magufuli ameahidi kujenga reli ya treni ya abiria kutoka Dodoma mjini hadi Bwigiri, lakini na sisi wanakongwa tunamuomba rais kujenga reli hiyo hadi Kibaigwa ambako kuna soko kubwa la mahindi ili kusogeza karibu huduma ya usafiri kwa wafanyabiashara wanaofika sokoni hapo,” amesema Zuberi

Pia Zuberi amesema reli hiyo itakapofika katika mji mdogo wa Kibaigwa itarahisisha usafiri kwa wananchi wa kawaida kwa kuwa hivi sasa kuna shida ya usafiri kati ya hapo na Dodoma mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!