August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kabila kushinikizwa kuachia ngazi mwaka huu

Joseph Kabila, Rais wa DR Congo

Spread the love

CHAMA cha Upinzani cha Union For Democracy and Social Progress (UDPS) cha DRC kimebainisha mpango wake wa kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani, anaandika, Catherine Kayombo.

Mpango huo utahusisha migomo na kutoendelea kuitii serikali ya rais Kabila na mpango huo taayari umetangazwa na chama hicho baada ya mazungumzo ya siku mbili.

Kwa mujibu wa msemaji wa upinzani, Francois Muamba wamepanga kufanya mgomo wa kitaifa kuanzia Agosti 8 mwaka huu.

Amesema maandamano hayo yatafanyika katika jiji kuu la Kinshasa na katika majimbo 25.

Muamba alieleza kuwa ikiwa Kabila hatotangaza tarehe ya uchaguzi kufikia mwishoni mwa Septemba mwaka huu, hatatambulika tena kama rais wa Jamhusi ya Demokrasia ya Congo ifikapo Oktoba mosi mwaka huu.

Uchaguzi mkuu nchini DRC ulitakiwa kufanyika mwaka huu chini ya mkataba unaokusudia kuepusha vurugu za siasa, lakini mpaka sasa tarehe ya uchaguzi haijajulikana baada ya rais kukataa kuondoka madarakani baada ya muda wake kuisha Desemba 2016,

error: Content is protected !!