Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madereva bodaboda wachongewa bungeni
Habari za Siasa

Madereva bodaboda wachongewa bungeni

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuweka mikakati ya kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya madereva wa pikipiki (bodaboda), ili kunusuru maisha ya wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 5 Februari 2024, bungeni jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu baada ya Mbunge wa Shaurimoyo, Ally Juma Mohamed (CCM) kuhoji Serikali ina mkakati gani kudhibiti ajali za bodaboda zinazogharimu maisha ya wananchi wengi.

“Suala la bodaboda ni kero kubwa hasa kwenye utumiaji wa sheria za barabarani, mimi ni mtetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali ambazo wanazifanya,” amesema Zungu na kuongeza:

“Lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha sababu Muhimbili ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana.”

Awali, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amelisema Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali ya kudhibiti ajali za bodaboda ikiwemo kutoa elimu na kutumia sheria kuwaadhibu wanaobainika kukiuka sheria za barabarani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!