Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka vigoli kuzuiwa kuingia disko
Habari za Siasa

Mbunge ataka vigoli kuzuiwa kuingia disko

Spread the love

MBUNGE wa Gando (CCM), Mussa Omar Salim, ameitaka Serikali kuweka mikakati ya kuzuia wimbi la wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kwenda katika klabu za usiku za starehe na miziki, ili kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu, Salim amedai kwa sasa ni ngumu kumjua msichana mwenye rika hilo kwa kumuangalia usoni kutokana na makuzi, kitendo kinachopelekea baadhi ya wanaume kuwatongoza na kujiweka katika mazingira ya kupata kesi za ubakaji.

Mbunge wa Gando (CCM), Mussa Omar Salim.

“Ulimwengu wa sasa wasichana walio wengi hata wavulana tunapokuwa katika hali ya ukuza ni ngumu sana muda mwingine kutambua umri wa mtu kwa kumuangalia usoni, niishauri serikali iweze kuweka  namna nzuri ya kutambua umri wa ndugu zetu katika kumbi za starehe,” amesema Salim na kuongeza:

“Wimbi limekuwa kubwa na msichana ni ngumu sana kumjua huyu kuwa yuko chini ya umri wa miaka 18 kwa kumuangalia usoni na inafikia mahali akiombwa namba huko tunawa-attack watu wanabaka hali ya kuwa sisi wenyewe tunawaachia wanafunzi kwenda kwenye kumbi za starehe, naomba hili lichukuliwe kwa umuhimu wake.”

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis, amemjibu akisema Serikali inaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan wamiliki wa kumbi za starehe kwa lengo la kuweka mikakati na mbinu jumuishi za kusimamia ulinzi na usalama wa mtoto.

“Serikali inasimamia utekelezaji wa Sheria ya Mtoto Na.21 ya mwaka 2009, kifungu cha 158 (1)(b) ambacho kinakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki shughuli za mikusanyiko ya usiku zikiwemo klabu na kumbi za starehe,” amesema Mwanaidi na kuongeza:

“Aidha, Serikali inaendelea kutoa elimu ya malezi na makuzi ya watoto ili kuwapa wazazi na walezi uelewa wa athari za kuwaacha watoto bila ulinzi hasa wakati wa usiku na kuwakumbusha wajibu wao wa kulea na kutunza watoto katika maadili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!