Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi
BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the love

Zaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS inayomiliki maabara ya upimaji wa sampuli za madini kwa kiwango cha kimataifa mkoani Geita.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamebainishwa jana tarehe 27 2023 na Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya MSALABS, Mugisha Lwekoramu wakati wa ufunguzi wa maabara hiyo.

Akizungumzia kuhusu teknolojia inayotumika katika maabara hiyo Lweramu amesema inatumia teknolojia ya kisasa ya upimaji wa sampuli kwa njia ya mionzi yaani (PhotoAssay) ambayo ni rafiki kwa utunzaji mazingira kwasababu haitumii kemikali au moto katika upimaji sampuli.

Lwekoramu amesema  maabara hiyo ni sehemu ya mapinduzi ya teknolojia kwa sababu inamwezesha mdau kupata majibu ya sampuli ndani ya saa mbili ukilinganishwa na teknolojia ya zamani ya kutumia moto na kemikali.

Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi huyo kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini na kumtaka kuendelea kufungua matawi mengine nchini.

Aidha, amewapongeza pia kwa kuweza kuajiri watanzania kwa asilimia 99.8 akiamini kuwa wafanyakazi hao wataendelea kujifunza utumiaji wa teknolojia hiyo na kutoa ujuzi huo kwa watanzania wengine.

Mavunde ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwatengenezea mazingira rafiki ya uwekezaji na kutoa ushirikiano kwa jinsi itakavyohitajika katika mnyororo mzima wa sekta ya madini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

error: Content is protected !!