Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi awacharukia viongozi wa mitaa
Habari za Siasa

Lukuvi awacharukia viongozi wa mitaa

William Lukuvi, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi (kulia waliosimama) akizungumza wananchi wa Ubungo
Spread the love

WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nchini, amekemea vitendo vya uonevu vinavyofanywa na viongozi wa serikali za mitaa kwa kushirikiana na matapeli kuwanyonya wananchi, anaandika Irene Emmanuel.

Akizungumza leo katika eneo la Kimara, Kilungule wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, alipokabidhi hati 4000 za ardhi kwa wakazi wa eneo hilo, amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuacha kutumia vyeo vyao vibaya.

“Baadhi ya viongozi wa mitaa mnatumia vibaya sana vyeo vyenu, mnauza mali za maskini, mnaotoa taarifa kwa matapeli kwamba mwenye kiwanja hiki kafa alafu mnatoa vibali wakati mnajua eneo hili ni bwana fulani na wakati ananunua mlitia sahihi.” amesema Lukuvi.

“Kesi nyingi ninazoona unakuta mtu amevamiwa shamba lake, lakini huyo mvamizi amesaidiwa na mwenyekiti wa mtaa yuleyule aliyetia sahihi kumuuzia mtu mwingine, hiyo tabia lazima ikome.” anaongeza.

Lukuvi, amewataka viongozi wa wilaya kufanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa katika umiliki wa viwanja na ujenzi na siyo kujenga kiholela.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!