October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lukuvi alilia wasaidizi wake waliofariki Ifakara

Spread the love

WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi amewapa pole ndugu na jamaa waliofiwa kwenye ajali iliyotokea jana tarehe 23 Februari 2019 Ifakara na kuua wafanyakazi tisa. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Katika salama zake za pole alizozitoa leo tarehe 24 Februari 2019 amesema, amestushwa na ajali hiyo kubwa kutokea.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero iliyotokea jioni ya leo huko Ifakara,” alisema Lukuvi.

Katika ajali hiyo watu tisa wamepoteza maisha na wengine wanne wamejeruhiwa.

Gari hilo lilikuwa limewabeba watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wameajiriwa na Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme -LTSP).

Watumishi hao walikuwa wanatoka katika Kijiji cha Kibegere kurudi Ifakara ambako walikwenda huko kikazi.

“Ajali hiyo imepoteza nguvu kazi ya taifa kwa vile wengi wao walikuwa vijana,” amesema Lukuvi na kuongeza;

“Kwa niaba ya serikali na watumishi wa Wizara ya Ardhi, kwa masikitiko makubwa, nawapa pole wafiwa wote wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na wapendwa vijana wetu.

“Ninawathibitishia kuwa serikali inafanya kila iwezalo kuokoa misha ya majeruhi na kuhakikisha miili ya marehemu wote inasafirishwa na kuzikwa kwa mujibu wa taratibu.”

Lukuvi amewaomba ndugu waliofiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.

“Namuomba Mungu awajalie majeruhi wapone haraka na roho za mrehemu zipate pumziko la milele. Amen”

error: Content is protected !!