October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lugola atinga Takukuru bila ‘jezi’

Spread the love
KANGI Lugola, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje ametinga katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara, amefika ofisini hapo leo tarehe 31 Januari 2020, kabla ya saa 1:30 asubuhi, akiwa nje ya ‘jezi’ yake iliyozoeleka (kaunda suti yenye bendera ya Tanzania).

Mara nyingi, baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Kangi alishona kaunda suti na kisha kuzibandika bendera ya taifa ikiwa ni sehemu ya mabadili ya muonekano wa suti zake baada ya kuukwa uwaziri.

Maendeo mbalimbali Lugola amekuwa akitumia kaunda suti za namna hiyo, sambamba na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa na gari yake ndogo, Lugola hakuingia moja kwa moja, aliiacha gari hiyo nje na kisha kubeba mkoba wake mweusi na ilani ya CCM mkononi huku akitoa tabasamu kwa mbali.

Baada ya Lugola kuhojiwa, atafuata aliyekuwa Thobias Andengenye, Kamishina wa Zimamoto na kisha ataingia kuhojiwa Jakob Kingu, aliyekuwa Katibu Mkuu ambapo mwisho atahojiwa Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

error: Content is protected !!