Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Mkuu Uingereza ajiuzulu, avunja rekodi ya mwaka 1827
KimataifaTangulizi

Waziri Mkuu Uingereza ajiuzulu, avunja rekodi ya mwaka 1827

Liz Truss
Spread the love

 

Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss leo tarehe 20 Oktoba, 2022 amejiuzulu uongozi wa chama cha Conservative na uwaziri mkuu baada ya kukumbwa na ukosoaji mkubwa kwenye sera yake ya kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika hotuba fupi aliyoitoa leo jijini London, Truss amesema inabidi kuondoka madarakani kwa ajili ya kuimarisha umoja wa chama chake cha Conservative kwa maslahi ya taifa.

Kiongozi huyo amekabiliwa na shinkizo kubwa kutoka ndani ya chama cha Conservative kufuatia sera ya kiuchumi ambayo imekosolewa.

Kujiuzulu kwake kumetokea muda mfupi baada ya kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya ndani Suella Braverman.

Hata hivyo, Truss ataendelea kuwa waziri mkuu hadi chama cha Conservative kitakapomteua kiongozi mwingine.

Kiongozi huyo amekuwa madarakani kwa kipindi cha siku 45 ambapo alimrithi Borris Johnson ambaye naye ahudumu katika nafasi hiyo hadi Julai 7 mwaka huu ambapo alitangaza kung’atuka.

Aidha, Truss amesema kwamba wakati chama cha Conservative kinamtafuta mrithi wake, ataendeela kutekeleza sera za kiuchumi kwa ajili ya taifa.

Mpango wake wa kupunguza bajeti ulitikisa soko la fedha na kupelekea chama chake cha Conservative kumshinkiza kuondoka madarakani.

Katika taarifa fupi, Truss amesema, “Tulikuwa na nia ya kuweka kiwango cha chini cha kodi, na kuimarisha ukuaji wa uchumi ili kuifanya Uingereza kuwa na ushindani mkubwa baada ya kuondoka Umoja wa Ulaya.”

“Natambua kwamba kulingana na hali ilivyo, siwezi kutekeleza kazi yangu ipasavyo kulingana na ahadi nilizotoa na matarajio ya chama cha Conservative. Kwa hivyo, nimezungumza na mfalme, na sasa natangaza kwamba najiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative.”

Kabla ya kujiuzulu, Truss amefanya mkutano na kiongozi Graham Brady, anayesimamia masuala ya siasa kuhusiana na uongozi na mabadiliko ndani ya chama.

Brady ni mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Conservative wasiokuwa na nafasi za uwaziri, na ambao wanaweza kuwasilisha barua za kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Kabla ya kujiuzulu, wabunge 17 walikuwa tayari wamesema kwamba wanamtaka Liz Truss ajiuzulu, na wabunge 100 walikuwa wameandika barua kwa kamati ya Brady wakisema hawana Imani naye na ni lazima ajiuzulu.

Liz Truss amekuwa ofisini kwa siku 45 pekee – muda mfupi zaidi wa waziri mkuu yeyote wa Uingereza. Waziri Mkuu wa pili aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi alikuwa George Canning, ambaye alihudumu kwa siku 119 baada ya kufariki mwaka 1827.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!