Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Nitakuwa kama Nyerere
Habari za Siasa

Lissu: Nitakuwa kama Nyerere

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameahidi kufuata nyayo za Mwalim Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa nchi hiyo endapo atakuwa rais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea). 

Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2020, kwenye mkutano wake wa kampeni katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Amesema, Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ni muasisi taifa hilo alipinga mamlaka makubwa aliyopewa na Katiba ya Tanzania.

Lissu amemnukuu Mwalimu Nyerere kwamba, katika uongozi wake alisema anaweza kuwa na mamlaka ya kuwa dikteta kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi.

Julius Nyerere, Hayati Baba wa Taifa

“Mimi nitakuwa rais aina ya Mwalimu Nyerere, kwa sababu mwaka 1978 alipokuwa anahojiwa na BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza) kuhusu mamlaka yake, alisema kwa mujibu wa Katiba na sheria ya nchi, mimi ninaweza kuwa na mamlaka ya kuwa dikteta,” amesema Lissu akimnukuu Hayati Nyerere.

Kwenye kampeni hizo, Lissu ameahidi kurejesha mchakato wa Katiba Mpya itakayorudisha mamlaka kwa wananchi.

“Nchi hii inahitaji Katiba mpya na katiba mpya ni mkataba wa wananchi, nitarudisha mamlaka ya wananchi, nitakuwa rais wa katiba mpya,” ameahidi Lissu.

Leo Ijumaa, Lissu anaendelea na kampeni mkoani Tabora.

2 Comments

  • Kubwa aliloasisi Mwalimu ni Azimio la Arusha na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Mnasahau hili halafu mnazungumzia mambo madogo ya katiba. Tuambie iwapo mtarejeshesha MIIKO YA UONGOZI ambayo imefutwa baada ya CCM kupitisha azimio la Zanzibar

    Vyama vya siasa acheni kutuzuga kuwa mnamuenzi Mwalimu. Ukweli ni kuwa mnamtumia ili kujipatia kura – si Chadema wala si CCM vyama vyote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!