Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo Kaze: Nimekuja kurudisha ukubwa, heshima Yanga
Michezo

Kaze: Nimekuja kurudisha ukubwa, heshima Yanga

Spread the love

KOCHA mpya wa Klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema, amekuja nchini Tanzania kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria nchini humo na kuirudishia hadhi na ukubwa unayoendana nayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Kocha huyo ambaye aliwasili nchini jana Alhamisi saa nne usiku na leo Ijumaa ameingia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo wa kukinoa kikosi chao kwa miaka miwili kunzia tarehe 15 Oktoba 2020 mpaka 15 Oktoba 2022.

Kaze amesema, Yanga ni timu yenye historia kubwa nchini na ameifuatilia timu hiyo katika michezo yote mitano waliocheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo yupo hapa kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo na kurudisha ukubwa wa timu hiyo.

“Kitu kilichonileta hapa ni kutumika klabu ya Yanga na ni timu yenye historia kubwa hapa na tunataka kurudisha ukubwa wa Yanga kwa sasa,” amesema Kaze ambaye ni raia wa Burundi.

Kaze amechukua nafasi ya Zlatko krmpotic aliyetumuliwa amesema “kitu cha kwanza nitakacho tanguliza ni wachezaji kwa sababu wao ndio watatupa matokeo na kutupatia furaha Wanayanga.”

Kuhusu aina ya mpira anaoutaka, Kaze amesema, anataka kuona wachezaji wakicheza na kupunguza mbwembwe kuwafurahisha mashabiki.

”Hatutaki mpira wa show, tunataka mpira wa kwenda mbele, hapa mnaita sijui kucheza na jukwaa, mimi sitataka hiyo, zaidi nataka timu ishinde sio mchezaji kuonyesha sifa binafsi. Siyo unapiga kanzu unarudisha mpira nyuma badala ya kwenda mbele,” amesema Kaze

Mara baada ya kuingia makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msolla amesema, ni jambo jema kumpata kocha ambaye walimkusudia kwa kuwa ndio chaguo sahihi na kuahidi kumpa ushirikiano na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kumpunguzia presha kocha huyo.

“Tunakukaribisha na kwa bahati nzuri timu unahifamu na wachezaji unawafahamu hivyo, sisi kama Yanga tumefurahi sana kwa ujio wako kwa kuwa wewe ndio chaguo sahihi, sisi kama klabu tutakupa ushirikiano asilimia mia,” amesema, Dk. Msolla

“Ni jambo jema kuwa na Mwalimu ambaye tulimkusudia kapatikana na sio jambo rahisi kumpata kocha hivyo, nawaomba mashabiki wa Yanga tumpunguzie presha mwalimu, tumuacha afanye kazi yake na naimani na yeya anataka matokeo” alisema Mwenyekiti huyo

Kocha huyo ambaye ataanza kukinoa kikosi hiko kuanzia kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa 22 Oktoba 2020 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Kaze amekuja Yanga kuchukua nafasi ya Zlatko krmpotic ambaye alidumu na timu hiyo kwa kipindi cha siku 37, licha ya kuingoza timu hiyo kwenye michezo mitano alifanikiwa kushinda minne na kwenda sare mchezo mmoja.

Kaze anamiliki lesseni daraja la kwanza ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) pamoja na leseni ya Chama cha soka Ujerumani Deustcher Fussball Band (DFB).

Aidha, kocha huyo ameshawahi kufundisha timu za Taifa za Burundi chini ya umri wa miaka 17, 20 na 23.

Pia, ameshafanya kazi kwenye akademi ya Barcelona.

Kaze amewahi kuwafunga Yanga mabao 2-0 wakati akiifundisha Atletico Olympic walipokutana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!