Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Shoo ahofia kutoweka amani
Habari za Siasa

Askofu Shoo ahofia kutoweka amani

Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dk. Frederick Shoo
Spread the love

DAKTARI Frederick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amekemea mamlaka na viongozi wa dini kupendelea chama kimoja cha kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, kiongozi huyo wa dini amekemea vitendo vya kupiga na kudhalilishwa kwa baadhi ya wagombea wakiwemo wanawake wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Amesema, vitendo hivyo vya udhalilishaji vikiendelea kumea bila kukemewa, vinaweza kusababisha kuhatarisha amani ya Taifa.

Askofu Shoo ametoa kauli hiyo jana Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2020 mbele ya waandishi wa habari baada ya kufungua mdahalo wa viongozi wa dini kuhusu kuhamasisha wanawake kwenye uongozi na ngazi za uamuzi.

“Unapoegemea waziwazi chama kimoja, tukijua hawa ni wanasiasa na siasa ni mchezo wa aina yake, kama viongozi wa dini, maandiko yanaelekeza vizuri kabisa namna ya kusimama na namna ya kuhitaji wote kuwashauri na kuwaombea.”

Mkurugenzi WiLDAF, Anna Kulaya

“Kama kuna mahali pa kukemea kutokana na ukiukwaji wote kwa pamoja, fanya bila ubaguzi na kuficha,” alisema Askofu Shoo.

“Tumekemea na kutahadharisha kwamba uvunjifu wa amani unaanza na jambo dogo kwa hiyo, si tu kudhalilisha wanawake, kuwapiga wagombea wa aina yoyote… Linapotokea jambo la namna hiyo, linagusa hisia za watu. Nasema mambo hayo ni ya kukemewa na kuachwa mara moja na jamii yetu,” alisema.

Askofu Shoo alisema “tumeshuhudia lugha nyingi za udhalilishaji wa wanawake katika kampeni zinazoendelea. Ni vyema mdahalo huu utoke na tamko moja la kukemea lugha za kashfa, kejeli na udhalilishaji kwa wanawake, hususani kipindi hiki cha kampeni.”

Mdahalo huo umeandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake (UN-Women.)

Kuhusu, baadhi ya viongozi wa dini nchi kuegea chama kimoja cha siasa, Askofu Shoo alisema, uamuzi huo unasababisha kuwagawa wananchi na waumini wao ambao wanatoka kwenye vyama mbalimbali.

Askofu Shoo alitaja mambo makuu manne ambayo viongozi wa dini wanatakiwa kusimamia wanapozungumzia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za uongozi na uamuzi, kuzuia migogoro isiyo ya lazima, kejeli, lugha za kashfa na udhalilishaji hususan kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.

Naye Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pwani, Alex Malasusa alisema “mimi ningependa twende na jinsia zote. Kwa sababu tukiendelea kuangazia upande mmoja, miaka kadhaa ijayo tutajikuta tunarudi katika kuwainua watoto wa kiume. Twende pamoja katika mabadiliko.”

Awali, Mkurugenzi WiLDAF, Anna Kulaya alisema “wanawake kushiriki katika uongozi ni haki yao ya kimsingi kama ilivyobainishwa katika mikataba mbalimbali. Lakini pia wana nafasi ya kufanya maamuzi yanayozingatia mahitaji ya kijinsia hasa ya kike.”

Anna alisema “katika dini kuna maandiko ambayo yameshushwa, wanawake hatuwezi kuyapinga. Tunaheshimu. Katika Misikiti na Makanisa sio lazima tuwe Maimamu na Mapadri, zipo nafasi za uongozi zingine. Hizo ndio tunazitaka.”

1 Comment

  • Ni aibu na hatari kuona kiongozi wa dini (sheikh au mchungaji) akisimama na kumpigia kampeni mgombea wa chama fulani. Wanadiriki hata kuhudhuria mikutano ya wagombea
    ACHENI UNAFIKI. Kama wewe una itikadi basi ni yako binafsi na wala si ya jumuiya ya kidini

    NCHI YETU HAINA DINI – NI WANANCHI NDIO WANA DINI.- KILA WANANCHI ANA HAKI YA KUABUDU APENDAVYO AU HATA KUTOABUDU DINI YOYOTE, – HII NI KWA MUJIBU WA KATIBA AMBAYO MUMEAPA KUILINDA NA KUITETEA – NCHI YETU NI SEKULA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!