May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu: Nitabadili mfumo

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania Bara, ameahidi kubadili mfumo wa kibiashara ili kuwaneemesha wananchi waliopo mipakani kiuchumi na kibiashara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Karagwe … (endelea).

Akizungumza na wakazi wa Kayanga, Karagwe mkoani Kagera amesema, zipo fursa mbalimbali kwa wakazi wa mipakani na kwamba, miongoni mwao ni kuuza bidhaa ikiwemo mazao nje ya nchi.

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho amesema, miongo ni mwa mambo yanayorudisha nyuma wakulima ni pamoja na kulazimishwa kuuzia mazao yao vyama vya ushirika.

“Mkulima wa kahawa hapa Karagwe wanaangushwa na vyama vya ushirika. Mkulima akilima mazao yake anaambiwa aweke kwenye gunia kwa kuwa, hawezi kuuza mpaka auzie chama cha ushirika ambacho badala ya kutoa fedha, kinawapa karatasi,” amesema Lissu.

Amesema, tatizo la sasa ni kwamba, wakulima wanalima kahawa yao kwa jasho lao, kisha wanakopwa na hata pale wanapopata malipo ya kahawa yao, bado wanakatwa fedha.

“Mnakopwa kahawa yenu halafu wakija kulipa wanawakata, utaratibu wa kukopa wakulima kahawa umewafanya kuwa masikini,” amesema.

error: Content is protected !!