December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar aahidi neema kwa walimu

Spread the love

ABOUBAKAR Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), amewahakikishia walimu kuwa Serikali inaendelea kulipa malimbikizo yote wanayodai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, ameonya walimu kutojihusisha na vitendo vya uvujifu wa mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba 2020.

RC Kunenge ametoa ahadi hiyo jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 alipofanya kikao kazi na mamia ya walimu wa Shule za Msingi zilizopo Wilaya ya Ilala kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili na kuangalia namna bora ya kuendelea kuboresha hali ya elimu.

Alisema Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili ikiwemo malimbikizo yote wanayodai ili kuhakikisha yanalipwa.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuonya walimu kutojihusisha na vitendo vinavyokiuka maadili ya usimamizi wa mitihani kwani hali itakayoweza chafua sifa nzuri ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Kunenge aliiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutoa ajira kwa walimu ili kutokomeza changamoto ya uhaba wa walimu

error: Content is protected !!