TUNDU Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaaam…(endelea).
Na kwamba, haijawahi kutokea uchaguzi ukawa rahisi lakini huu ni mgumu zaidi akihusisha hali ya kisiasa, mazingira ya upatikanaji wa fedha na miaka mitano ya utawala wa Rais John Magufuli.
Akizungumza na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Septemba 2020 amesema, kazi ya kuuondoa utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni kubwa.
“Hatujidangani kwamba kazi ni nyepesi, kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa kweli kweli. Nimeshiriki chaguzi tangu mwaka 1995 na mbili nilishinda, nafahamu jinsi uchaguzi wa Tanzania ulivyo mgumu kwa chama chochote cha upinzani.
“Nafahamu ilivyo vigumu kuishinda CCM. Hatujidanganyi kwamba mara hii ikwa rahisi, haijawahi. Mfumo wetu wa uchaguzi umejengwa kuipendelea CCM,” amedai Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
Mgombea huyo ameeleza kuwa, uchaguzi unakuwa mgumu kwa mambo kadhaa akieleza kwamba miongoni mwayo ni watumishi wanaoshughulika na uchaguzi kuwa ‘wateule’ wa mgombea kutoka chama tawala.

“Mwenyekiti wa tume (Tume ya Uchaguzi) wanateuliwa na rais, msaidizi wake anateule na rais, wasaidizi na wakurugenzi ni wateule wa mgombea wa CCM.
“Wanaweza kuondolewa wakati wowote na rais. Mfumo wa uchaguzi bado ni mgumu, maaskari, usalama na mfumo mzima wa serikali hawapo upande wetu. Tunaamini Watanzania wapo tayari kufanya mabadiliko kweli kweli,” amesema.
Amesema, yeye kama mgombea anaelewa Watanzania wanahitaji ninin kwamba, kikubwa ni kubadilisha mfumo wa kitawala ulioachwa na wakoloni.
Leave a comment