Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu ahusisha ujenzi wa kanisa na maisha ya jamii
Habari Mchanganyiko

Askofu ahusisha ujenzi wa kanisa na maisha ya jamii

Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Power of God Fire, Dankton Rweikila amesema unapojenga nyumba ya Mungu ni mbegu ambayo inapandwa ndani ya jamii na kusababisha watu kuwa na hofu ya Mungu jambo ambalo linaleta furaha, upendo na amani katika nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Rweikila aliyasema hayo Jumapili iliyopita alipokuwa kwenye ibada ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo hilo lililopo Chanika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Alisema jamii inapojenga nyumba ya Mungu inapanda mbegu ambayo kizazi hadi kizazi kinakuwa na hofu ya Mungu ambapo wataogopa kufanya maovu  matokeo yake nchi inakuwa na maendeleo.

Rweikila alisema kanisa linajengwa na mtu anayetambua kuwa Mungu yupo lazima iwe sehemu maalumu ya kumwabudia na yeyote anayejenga nyumba ya Mungu  sadaka ina nguvu katika maisha yake ikiwemo familia, kazi ya mikono na inamlinda kwa kumuepusha na magonjwa,l aana na mauti.

“Mtu anayejitoa kwa hili akatoa sadaka yake, anaandaa ulinzi katika maisha yake hivyo leo tumeweka nguzo kwenye nyumba ya Mungu jambo hili tunamshukuru ametutendea mengi hasa ugonjwa wa corona ametuvusha kuliko nchi zingine,” alisema Rweikila.

Alisema kuna baadhi ya nchi bado zinateseka na ugonjwa huo lakini Tanzania imepata upendeleo wa ajabu ambayo imevushwa pasipo maangaiko yeyote.

Rweikila alisema, Rais John Magufuli akasikia wito ndani yake akatangaza siku tatu ya maombi ambapo kanisa hilo ni miongoni lililoombea Taifa ili liondokane na janga hilo.

Muumini wa kanisa hilo, Getrude Michaila alisema waumini wazidi kujitolea ili kanisa hilo liweze kusimama hivyo wanapojitolea wanapata hazina mbinguni Hadi kizazi na kizazi.

“Tukio la leo linanifundisha mambo mengi ninapanda hii mbegu hadi kizazi changu hivyo familia yangu itakuwa vizuri Kwa kumpendeza Mungu,”alisema Michaila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!