Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu awajibu wanaosema ameanza kampeni mapema
Habari za SiasaTangulizi

Lissu awajibu wanaosema ameanza kampeni mapema

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Mgombe urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, madai yanayotolewa kuwa atapingwa kwa kufanya kampeni kabla ya wakati ni ya kupuuzwa kwani hayana msingi wa kisheria. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea)

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumapili tarehe 23 Agosti 2020 Makao makuu ya chama hicho Ufika jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara amesema, kwenye sheria hakuna kosa la kufanya kampeni kabla ya muda.

“Nasikia kuna kelele za kwamba mnafanya kampeni kabla ya wakati mtawekewa pingamizi, hayo ni makelele kwenye sheria zetu za uchaguzi hakuna kitu kinachoitwa kosa la kufanya kampeni kabla ya wakati,” amesema Lissu.

Lissu amesema alichofanya yeye na Mgombea mwenza wake, Salum Mwalim ni kuwaeleza wananchi kuwa wanastahili kuchaguliwa.

“Tulichokionesha sisi kwa siku 12, kuonesha tunavyostahili kuchaguliwa wala sio kampeni kwa hiyo hayo makelele mnaweza kuyapuuza kwa jinsi yanavyostahili kupuuzwa,” amesema Lissu.

Lissu ameeleza kuwa yeye na Mgombea Mwenza wake walifanya ziara kwenye mikoa 16 tanzania bara kutafuta wadhamini.

“Mimi na mgombea mwenza wangu tulifanya ziara kwenye mikoa 16 tanzania bara, tulianzia Dodoma, tumekwenda Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga Morogoro,Iringa Mbeya Songwe na Njombe.”

“Katika mikoa yote hiyo tumefanya mikutano mikubwa na wananchi vyombo vya habari vya kwetu hasahasa magazeti na Televishion havikuona mikutano hiyo  kwa hiyo haijaonesha chochote, lakini ukiingalia mtandao utajua jinsi gani ambavyo mamia na maelfu ya watanzania wamehudhuria mikutano hiyo,” amesema Lissu

Amesema, mikutano aliyoifanya kwenye ziara zake imemtia moyo na kwamba Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko.

“Mikutano hiyo inaonesha kwamba Watanzani wapo tayari kwa mabadiliko makubwa ya kisiasa ya uchaguzi Mkuu. Watu hawakuja kumshangaa huyu aliyepona kwa risasi 16, wamekuja kumuona kiongozi ambaye wanamfahamu na wanamfahamu kwa miaka mingi kwa sababu licha ya matatizo makubwa aliyepitia bado amesimama imara kutetea haki za nchi hii, maslahi ya nchi hii hawakuja kunishangaa kama alivyosema mtu fulani,” amesema.

Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria ameswmq “Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na hawatakuwa tayari kufanyiwa mchezo mchezo kwenye uchaguzi huu.”

Jumla ya wagombea 17 wamechukua fomu za uteuzi wa urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na tarehe 25 Agosti 2020 itafanya uteuzi wa wagombea waliokidhi vigezo.

Baada ya uteuzi, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!