Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi yawadaka 12, tuhuma kuvuruga mkutano wa Lissu
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Polisi yawadaka 12, tuhuma kuvuruga mkutano wa Lissu

Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linawashikilia watu 12 Wilaya ya Hai kwa mahojiano wakituhumiwa kufanya vurugu na kushambulia kwa mawe mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu alipokuwa akitafuta wadhamini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Vurugu hizo zilitokea tarehe 14 Agosti 202  wilayani Hai ambapo zilisababisha majeruhi wanne waliojeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa hospitali ya Wilaya hiyo.

Katika vurugu hizo, baadhi ya magari yariharibika kutokana na kupondwa kwa mawe.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jumapili 23 Agosti 2020, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Emmanuel Lukula amesema, jana Jumamosi ulifanyika msako mkali na kuwakamata watuhumiwa hao ambao kwa sasa wanahojiwa na watafikishwa mahakamani.

”Nitoe wito kwa wananchi na wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu hasa tunapoelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu zitakazoanza 26 Agosti 26, 2020,” amesema Lukula

”Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro tumejipanga kuhakikisha amani zinatawala wakati wote kwa atakayeenda kinyume na sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi tutakabiliana naye kwa nguvu zote na bila huruma kwa mujibu wa sheria,” amesema Lukula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!