Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu amweka mtegoni Rais Samia kuhusu miradi ya JPM
Habari za SiasaTangulizi

Lissu amweka mtegoni Rais Samia kuhusu miradi ya JPM

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amemshauri Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aipige chini miradi ya maendeleo, isiyokuwa na tija kwa Taifa, aliyoirithi kutoka Serikali ya Hayati John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …  (endelea).

Lissu ametoa wito huo leo Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2021, akitoa salamu zake za kuuaga mwaka huo, kwa njia ya mtandao.

“Rai yangu kwa Rais Samia na Serikali yake, apate ujasiri wa kisiasa wa kuiangalia miradi yote hii upya na kuamua kama kuna manufaa yoyote ya kiuchumi na kijamii kuendelea nayo kwa muundo wake wa sasa. Akijiridhisha kwamba haitekelezeki bila kuifilisi nchi yetu, kama ushahidi huru unavyoonyesha, basi awe na ujasiri wa kuachana nayo,”amesema Lissu.

Mwanaisasa huyo amedai kuwa, asipofanya hivyo, utekelezwaji wa miradi hiyo huenda ukakwama.

“Asipofanya hivyo, tena kwa haraka, kuna hatari kubwa mbeleni ya miradi hii kuwa magofu ambayo hayatakamilika. Rais Samia apate ujasiri wa kuwaambia Watanzania ukweli mchungu badala ya kuendelea na maneno matamu kama ‘kazi iendelee’, kama ilivyokuwa ‘hapa kazi tu’ ya mwendazake,” amesema Lissu.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Lissu amesema “ni bora kupata aibu kwa kusema ukweli na kupunguza hasara, kuliko kupata laana ya kuwadanganya wananchi na kuliongezea taifa mzigo mkubwa zaidi , wa madeni na hasara zinazoepukika.”

Mwanasiasa huyo ametoa mfano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, unaogharimu matrilioni ya fedha, akisema kuwa, haukupaswa kutekelezwa kwa kuwa unachukua muda mrefu huku nchi ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa umeme.

Lissu amedai kuwa, fedha hizo zingepelekwa katika miradi mikubwa na ya kati ya nishati mbadala, kama upepo na jua, inayotekelezwa kwa muda mfupi.

“Wakati tukiendelea kumwaga matrilioni haya katika mradi huu, tunaendelea kukabiliwa na matatizo makubwa ya mgawo wa umeme kila mahali nchini. Kama hawa wanaojiita watetezi wa wanyonge wangeamua kuwekeza matrilioni hayo, katika miradi mikubwa au ya kati ya nishati mbadala za jua au upepo au gesi asilia,” amesema Lissu na kuongeza:

“Ambazo zina uwezekano mkubwa wa kutatua matatizo ya nishati katika nchi yetu, gharama zake zingekuwa nafuu zaidi, huku muda wa kukamilisha miradi hiyo ikiwa kati ya mwaka mmoja hadi miwili. Ukweli ni kwamba wakati wa utawala wa Rais Jakata Kikwete kulitengenezwa mpango mkakati wa nishati ambao ulilenga kuendeleza miradi ya aina.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!