Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu amuunga mkono Spika Ndugai
Habari za Siasa

Lissu amuunga mkono Spika Ndugai

Job Ndugai
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amedai kuwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikosea kusema kuna siku nchi itapigwa mnada kutokana na madeni, kwa kuwa tayari ilishapigwa mnada. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo lo Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2021, akitoa salamu zake za kuufunga mwaka huo, kwa njia ya mtandao.

Mwanasiasa huyo aliyeko ughaibu nchini Ubelgiji, amedai kuwa, hakuna mtu anayefahamu masharti ya mikopo iliyochukuliwa na Serikali.

“Sio Bunge wala Watanzania kwa ujumla wetu, tunaojua masharti ya mikopo hii, ila tunajua tutailipa yote na riba juu tutake tusitake! Kwa hali hii, Spika Ndugai alikosea aliposema kuna siku nchi yetu itapigwa mnada, imeshapigwa mnada tayari, tena siku nyingi ila bado hatujajua bei yote ya mnada huo,” amedai Lissu.

Lissu amedai kuwa, deni la Taifa linakua huku kukiwa hakuna dalili ya Serikali kusitisha ukopaji.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

“Sasa tunaambiwa kwamba deni la taifa limefikia zaidi ya Sh. 70 trilioni na malipo ya riba kwa deni hilo pekee ni zaidi ya Sh. 10 trilioni kwa mwaka. Tukumbuke kwamba, hizi ni pesa zinazolipwa kwa mikopo kwa ajili ya miradi ambayo bado haijakamilika na kuanza uzalishaji,” amedai Lissu.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, mwaka huu Serikali imekopa Dola za Marekani 2.5 bilioni (Sh. 6.245 trilioni)

“Ulevi huu wa mikopo hauelekei kwisha au kupungua, hata baada ya mwendazake kwenda zake. Kwa taarifa zilizopo, kwa mwaka huu peke yake, Serikali yetu imekopa dola milioni 875 (Sh. 2.2 trilioni) Mei, kutoka Benki ya Dunia (W.B). Dola milioni 150 (Sh. 375 bilioni) kwa ajili ya Zanzibar mwezi Juni kutoka WB,” amedai Lissu.

Lissu amedai “dola milioni 567 (Sh. 1.4 trilioni) mwezi Septemba kutoka IMF, dola milioni 256 (Sh. 640 bilioni) kati ya Mei na Septemba kutoka AfDB, na dola milioni 650 (Sh. 1.6 trilioni ) kutoka WB mwezi huu pekee.”

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM

Spika Ndugai alitoa kauli hiyo ya kwamba ipo siku nchi itapigwa mnada kutokana na kuelemewa na madeni, jijini Dodoma, tarehe 27 Desemba 2021, baada ya Serikali kuchukua mkopo wa Sh. 1.3 trilioni, kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa ajili ya kukabiliana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).

Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan, alisema Serikali yake itaendelea kukopa fedha kwa ajili ya kumaliza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hivi karibuni, baada ya mjadala wa deni la taifa kupamba moto, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema deni hilo ni himilivu kwa kiwango kikubwa.

3 Comments

  • Asante ndugu lissu makamo mwenye kiti hewa wa chadema lolote usemalo wale watacheka na kukkuona bure natena hauna uwezo wa kuongea yenye maana uongozi ni tabia njema yenye ukweli endelea kutimiza wajibu wako wakuongea habari hewa

  • Asante lisu kwa mawazo mazur kutuhabalisha kuwa inch imeuzwa pia asante ndugai kutujulisha kuwa inch itapigwa mnada kweli tunaona deni kubwa huku wanasema kukopa ni lazima nimuombe spika wabunge atusaidie niwaombe wana ccm wenzangu tusimubeze ndugai ametujulisha habali njema asante ndugai mungu akutangulie

  • Lissu, huo mradi wa Umeme ukikamilika tatizo la umeme litakwisha. Bado kuna haja ya kuukamilisha kwa wakati vingievyo ni hasara za kujitakia. Hasara itaonyesha ujinga wetu.
    Nishati mbadala ni baada ya umeme. Hatuna mtandao wa kusambaza gesi. Tutumie chuma chetu cha mchuchuma na liganga kutengeneza mabomba wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!