Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Limeni kilimo kinachohimili mabadiliko tabia ya nchi’
Habari Mchanganyiko

‘Limeni kilimo kinachohimili mabadiliko tabia ya nchi’

Shamba la mihogo
Spread the love

WAKULIMA nchini wametakiwa kutumia ardhi ndogo ya kilimo waliyonayo, kuzalisha kwa tija na kufikia malengo ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia nchi (CSA). Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mtafiti mwandamizi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA), Dk. Freddy Baijukya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari za Kilimo, Sayansi na Teknolojia Tanzania (TAJF), uliofanyika kwa ufadhili wa Shirika la Msaada la Marekani (USAID).

Dk. Baijukya amesema, matumizi ya ardhi ndogo kwa kilimo chenye tija yatasaidia mkulima kuweza kuzalisha mazao, ikiwemo mahindi kwa wastani wa tani 2.5 kwa hekta kiasi ambacho hakijafikiwa hata nusu yake mpaka sasa. 

Amesema, wamejipanga kuelimisha wakulima juu ya CSA inavyoangalia na kuondoa madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza uzalishaji wenye tija.

Pia kuzingatia uvumilivu kwenye mabadiliko ya tabianchi sambamba na kupunguza uzalishaji wa gesi za kijani, ikiwemo gesi ya ukaa jambo litakalomsaidia mkulima.

Na kwamba, licha ya ufugaji na kilimo kuonekana chanzo cha mabadiliko ya tabia nchi, lakini ndio sehemu ya uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hivyo, ni vema malengo na sera yaliyowekwa na Serikali yaweze kutekelezeka.

“Mfano eneo la Iringa uzalishaji wa zao la Pamba umeshuka kutokana na wanawake kususa kupalilia, kwasababu wanaume wanalala hoteli miezi mitatu baada ya mauzo na kurejea nyumbani wakiwa hawana kitu,” alisema.

Dk. Baijukya amesema, kumsaidia mwanamke kuendeleza kilimo kunaweza kufanikiwa kwa kuleta mashine rahisi zitakazomsaidia na hivyo kumpa nguvu ya kuendeleza kilimo nchini.

Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo Kitengo cha Mazingira, Evelyn Kagoma amesema wizara imeendelea kuandaa sera na mipango mbalimbali ya kusaidia wakulima, ikiwemo kufanya urutubishaji wa ardhi na upatikanaji wa maji kwenye maeneo ya kilimo.

Aliitaja mipango mingine kuwa ni kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kwa kufuata mwongozo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi uliozinduliwa rasmi mwaka 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!