Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: CCM ipo hoi, wanachama 90 wamfuata
Habari za Siasa

Zitto: CCM ipo hoi, wanachama 90 wamfuata

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kiko hoi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Zitto ametoa kauli hiyo wakati akiwapokea wenyeviti wa serikali za mitaa zaidi ya 90, kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) leo tarehe 22 Oktoba 2019 jijini Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo kufuatia agizo la Dk. Bashiru Ally, la kurudia mchakato wa kura za maoni katika maeneo ambayo yaliyokuwa na dosari na kusababisha malalamiko.

“CCM unaona wanagombana, jana tumeona katibu wao anazungumza wanataka kutoana manundu. CCM wako hoi. Ni lazima tuungane kuitoa madarakani,” ameeleza Zitto.

Akizungumzia kuhusu zoezi la ugawaji kadi za ACT-Wazalendo kwa wenyeviti hao, Zitto amesema baadhi ya wenyeviti aliowapokea, hawakutendewa haki katika mchakato wa kura za maoni wa kuteua wagombea wa CCM kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019.

“Tumekabidhi kadi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa, ambao wametoka CCM jumla ya 52, ambao wao walikuwa na kura zao za maoni. Kuna watu ambao hawakutendewa haki, wameonewa, wameona bora kuja katika chama chetu,” amesema Zitto.

Wakati huo huo, Zitto amesema ACT-Wazalendo imejiandaa kusimamisha wagombea katika mitaa na vijiji vyote.

“Mpaka sasa tumejiandaa kuweka wagombea katika mitaa na vijiji vyote  viongozi wetu waelewe hivyo mpaka watakapo pewa maelekezo mengine na chama,” amesema Zitto.

Zitto ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuketi pamoja ili kupanga utaratibu wa namna watakavyoshirikiana katika uchaguzi huo.

Aidha, Zitto amewataka baadhi ya viongozi wa vyama vya pinzani kutorubuni wagombea wa chama chake, kwamba kuna utaratibu wa kuachiana maeneo, kwani bado hawafika makubaliano kuhusu suala hilo.

“Tunafahamu kuna haja ya kuweka ushirikiano, hakuna haja ya kupambana na CCM bila ya kuwa na umoja. Wito ni kuhakikisha tunakutana mara moja, ili kuweka utaratibu wa namna gani tunafanya.Lakini, mpaka sasa hakuna makubaliano ya kushirikiana, kila chama kinaweka utaratibu wa kugombea,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wako watu wanasema kuna maeneo ya kuachiana. Viongozi tukikaa mezani, utaratibu utatolewa na kwa hakika chama chetu kinahitaji ushirikiano na kuachiana kwa makubaliano. Kama haitakuwa tutaendelea kujiandaa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!