April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JNHPP yahamasisha uhifadhi misitu endelevu

Moja ya misitu iliyopo Tanzania

Spread the love

MRADI wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), utaweza kuwa endelevu endapo uhifadhi na utunzaji wa misitu hasa ya vijiji utakuwa endelevu na shirikishi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Charles Leonard, meneja mradi wa m kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa Tanzania (TTCS) alipokuwa kwenye wa mkutano wa maofisa mawasiliano wa wizara zinazojihusisha na misitu uliofanyika mjini Morogoro.

Leonard amesema, ni vema serikali ikahamasisha jamii kuhifadhi misitu ya vijijini ili miradi ya maendeleo inayohitaji kuwa endelevu iweze kuendelea.

Amesema, mradi wa TTCS  umeshirikisha wananchi wa vijiji 30 vya wilaya za Kilosa, Mvomero na Morogoro kwa kuhifadhi misitu kwa mfumo endelevu, na matokeo yake yamekuwa na faida.

“Mradi wa JNHPP hauwezi kuwa endelevu iwapo misitu itaisha. Njia ya kuiendeleza ni serikali kushirikiana na sisi wadau na wanakijiji kuitunza misitu, itafanya asilimia 45 ya misitu yote kuwa endelevu,” amesema.

Amesema, faida za mradi huo ni nyingi ambapo tangu uanzishwe mwaka 2012 hadi sasa, umeshawezesha vijiji kuingiza zaidi ya Sh. 3 Bil sambamba na kuimaridha uhifadhi.

Akitoa mada kwenye kikao hicho, ofisa mahusiano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Bettie Luwuge amesema, lengo la kukutana na maofisa mawasiliano hao ni kufanya kuwa na kauli moja ya uhifadhi wa mazingira.

error: Content is protected !!