October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lijuakali ajivunia kuijenga Chadema

Peter Lijualikali, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero

Spread the love

PETER Lijuakali, mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilipaswa kumshukuru kwa kuwa ndiye aliyekijenga Kilombero, Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini leo tarehe 23 Julai 2020 amesema, kama Chadema imemtoa mbali, basi na yeye ameitoa Chadema mbali hivyo wametoana mbali.

Amesema, Chadema haikuwa kwenye ramani ya wakazi wa Kilombero na kwamba, kauli kuwa yeye ndiye anayepaswa kukishukuru chama hicho haina maana.

        Soma zaidi:-

“Mimi nimefanya mambo ambayo yameiweka Chadema kwenye ramani Kilombero, moyo wangu, mikakati yangu, akili yangu, ushupavu wangu ndio zimefanya Chadema imekaa kwenye ramani ambayo ipo pale,” amesema Lijualikali

Mwanasiasa huyo kijana ni miongoni mwa waliokuwa wabunge wanaotokana na Chadema, alihama chama hicho na kujiunga na CCM, hata hivyo ameshindwa kupenya mbele ya mtia nia mwenzake Abubakari Asenga katika jimbo hilo la Kilombero.

Peter Lijualikali (kushoto) akipokea fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM

Amesema, kwenye tatizo kubwa lilijikita kwenye mtazamo wa kutoana mbali “hapa ndipo palipo na tatizo. Wanaohama CCM kwenda vyama vingine hawaambiwi wewe tumekutoa mbali.”

Amedai, dhana ya kutoana mbali ilianzishwa ndani ya chama hicho ili kuzima hisia za kuhoji baadhi ya mambo ambayo yalionekana kutokwenda sawa.

error: Content is protected !!