October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo tisa Takukuru wasimamishwa kazi

Brigedia Jenerali, John Mbungo

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imesimamisha kazi watumishi tisa waliohusika katika usimamizi wa ujenzi wa majengo saba ya ofisi za taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 jijini Dodoma na Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru wakati akizungumza na wanahabari.

Brigedia Mbungo ametoa taarifa hiyo wakati akizungumzia hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo kuhusu ubadhirifu uliofanywa katika ujenzi wa ofisi zake.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni wale waliosimamia ujenzi wa ofisi za Takukuru katika Wilaya za Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

Brigedia Mbungo amesema, Takukuru imeunda Tume Huru yenye wajumbe wanne kutoka nje ya taasisi hiyo, kwa ajili ya kuchunguza sakata hilo.

“Nimeunda tume huru toka nje ya Takukuru itakayochungua thamani ya fedha kwa majengo yote saba, pamoja na kuchunguza iwapo ubadhirifu, wizi, rushwa na matumizi mabaya ya hela za serikali yalikuwepo katika ujenzi hao, itakua na wajumbe wanne kutoka maeneo tofauti,” amesema Brigedia Mbungo.

 Taasisi hiyo imechukua hatua hiyo siku moja baada ya Rais John Magufuli kuitaka Takukuru kujitathimini utendaji wake.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana tarehe 22 Julai 2020 wakati anazindua Ofisi za Takukuru wilayani Chamwino,  baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa ofisi hizo, ambapo alisema gharama zilizotumika hazilingani na majengo husika.

error: Content is protected !!