December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kumekucha! Harmonize awavuruga WCB

Naseeb Abdul 'Diamond Platnum’

Spread the love

 

SIKU chache baada ya Msanii wa Bongofleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize au Konde Boy kutema cheche kuhusu mapito na changamoto alizokumbana nazo pindi akiwa chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), baadhi ya viongozi na wafuasi wa lebo hiyo wameanza kutafutana. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Harmonize alishusha tuhuma mbalimbali kwa mkali mwenzie aliyekuwa bosi wake katika lebo hiyo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ punde tu baada ya kutua nchini akitokea Marekani alikokuwa kwenye tour ya matamasha mbalimbali.

Harmonize alieleza mambo mengi hasa vitimbi alivyokuwa akifanyiwa katika lebo hiyo hadi kufikia uamuzi wa kujiengua na kufungua lebo yake ya Konde Gang.

Alisema baada ya kutoka, wafuasi wa Mondi wakiwamo wafanyakazi kama vile Babalevo wamekuwa wakimtukana lakini Mondi hachukui hatua yoyote. 

Kufuatia madai hayo, Meneja wa Mondi ambaye pia ni Mbunge wa Morogoro vijijini, Hamis Taletale au Babutale amesema tatizo kubwa ni uchonganishi unaofanywa na wapambe maarufu kama chawa ambao ni Mwijaku, Babalevo na Jumalokole.

Amesema ‘chawa’ hao ndio wanaosababisha kuharibu sanaa  ya Tanzania.

“Tuwashawishi hawa wasanii wafanye vizuri tupinge hawa wagombanishi wachache Mwijaku, Babalevo, Jumalokole hawa ndio wapumbavu tuwatoe hawa kwenye industry yetu, tu-ssuport muziki wetu tuache dhana” amesema Babutale alipokuwa akizungumza na chombo kimoja cha habari.

Harmonize

Babutale pia ameongezea kwa kusema kama angelikuwa na nafasi angewasimamisha wasifanye wanachokifanya kwani wasanii wanahitaji pongezi na sio kupondwa.

Aidha, kufuatia kauli hiyo ya Meneja wa Mondi, Babalevo hakubaki nyuma aliamua kumjibu bosi huyo wa WCB kupitia ukurasa wake wa Instagrama.P

Babalevo ameandika hivi, “Sijawahi kuona ‘mpumbavu’ kama wewe Babutale, unatuita wapumbavu ili tukujibu ukimbilie polisi,  nani kakudanganya ukiwa mbunge unamamlaka ya kutukana watu waziwazi tena hadharani!.”

error: Content is protected !!