Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Penalti ya Fei Toto, Simba wataka uchunguzi ufanyike
MichezoTangulizi

Penalti ya Fei Toto, Simba wataka uchunguzi ufanyike

Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba
Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Simba, umevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza tukio la penalti lilitokea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya Namungo dhidi ya Yanga, mara baada ya kuzua sintofahamu kubwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ulipigwa jana mkoani Lindi, kwenye Uwanja wa Ilulu ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo, Mwamuzi Abel Willium kutoka mkoani Arusha, alitoa penalti ya utata mara baada ya kutafsiri kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum “Fei Toto” kwamba alifanyiwa madhambi, huku kwenye picha za marudio zikionesha hakukukuwa na madhambi yoyote.

Licha ya mwamuzi huyo kutoa penalti hiyo, lakini pia alitoa kadi ya pili ya njano na kisha kumpa nyekundu kwa mchezaji wa Namungo na kufanya timu hiyo kucheza wakiwa pungufu.

Mwamuzi huyo pia, aliruhusu penalti hiyo kupigwa huku kukiwa na idadi kubwa ya wachezaji ndani ya boksi kinyume na kanuni na sheria.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza tukio hilo kwa kuwa yakiachwa yanaweza kuleta maafa.

“Sijawahi kuona katika maisha ya soka, penalti inapigwa na watu nane, tunataka vyombo vya usalama kuchunguza kwa kina haya mambo yanaweza kuleta maafa,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo, aliendelea kusema jambo hilo haliwezi kuvumulika wala kukubalika na kusisitiza kuwa hawawezi kuwashinda.

“Zipo sheria zinasimamia mpira, haiwezekana ili ni jambo ambalo halikubaliki, sisi hawawezi kutushinda wamepigwa hapa na wamepigwa nje, sisi tunashinda nyumbani na ugenini,” alisema.

Mwenyekiti huyo pia hakuishia hapo, aliendelea kusema, wao kama Simba hawafanyi mipango nje ya uwanja kwa kuwa wanaamini kwenye kucheza mpira uwanjani, na kuendelea kuamini kuwa Ligi ya msimu huu wameanza vizuri.

“Mwaka jana tulianza ligi vibaya, ila mwaka huu hatujaanza vibaya tumecheza mechi sita, tumeshinda minne, tumetoka sare mara mbili na hatujapoteza mchezo hata mmoja.

“Timu yetu Simba tunasimama mbele ya hadhara kwa wale tunaoshindana nao, kwamba hatufanyi mipango nje ya uwanja, tucheze mpira uwanjani,” alisema mwenyekiti huyo.

Mpaka sasa klabu hiyo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 14, nyuma ya Yanga ambao ni vinara kwenye msimamo huo wakiwa na pointi 16.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!