Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Sindano mbadala ARVs yaidhinishwa, wenye VVU wanachomwa mara 6 kwa mwaka
Kimataifa

Sindano mbadala ARVs yaidhinishwa, wenye VVU wanachomwa mara 6 kwa mwaka

Spread the love

 

TAASISI ya Usimamizi wa Dawa nchini Uingereza (NHS) pamoja na mashirika mengine ya msaada imeidhinisha matibabu  ya sindano mpya yenye ufanisi wa muda merefu kwa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Sindano hiyo husitisha makali ya VVU sawa na dawa za kawaida za kufubaza makali ya VVU – antiretroviral maarufu kama ARVs

Inakadiriwa kuwa watu 13,000 nchini Uingereza wanaweza kuamua kudungwa sindano hiyo badala ya kumeza vidonge hivyo kila siku.

Dawa hiyo ya sindano inayotengenezwa na ViiV Healthcare inafahamika kama Cabotegravir au Vocabria wakati inayoitwa Rekambys inatengenezwa na kampuni ya Janssen.

Sindano hiyo hutolewa mara mbili kwa muda tofautii kila baada ya miezi miwili.

Tiba hiyo ni bora tu kwa wale ambao wamefanikiwa kufikia viwango vya kutogundulika kwa virusi katika damu yao wakati wanapomeza vidonge.

Wataalamu wanasema tiba hii ya sindano inaweza kuwa rahisi na kutumiwa na wengi.

Profesa Chloe Orkin, ambaye ni mtaalam wa VVU kutoka Chuo kikuu cha Queen Mary cha London, amesema itawapunguzia mzigo watu wenye VVU ambao wamekuwa wakilazimika kumeza vidonge kila siku na badala yake kuwapatia tiba mara sita tu kwa mwaka.

Dk. Sanjay Bhagani, rais taasisi ya tiba ya Ukimwi – European Aids Clinical Society, amesema “Hili limepokelewa vyema kabisa.

“Bado unyanyapaa umebaki kuwa changamoto kwa jamii ya watu wenye VVU, na kumeza tembe kila siku ni jambo linaloweza kuwa gumu miongoni mwa baadhi ya watu. Hii inatoa tiba mbadala ya sindano kwa wengi.

“Takwimu na tafiti zinazoshauri tiba hii ni imara na uzoefu halisi wa dunia unaonyesha kwamba wagonjwa wanaoanza kwa tiba za sindano hupendelea kuendelea nazo.”

Alex Sparrowhawk, kutoka Manchester, anafanya kazi katika shirika la msaada linalowasaidia wanaoishi na VVU linaloitwa Terrence Higgins Trust.

Alibainika kuwa na VVU miaka 12 iliyopita na amekuwa akipokea dawa za ART tangu wakati huo. Anasema kuwa na chaguo tofauti la tiba ni jambo la kufurahisha.

“Habari hii mpya ni kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakikisubiri.

“Wazo la kudungwa sindano mara sita kwa mwaka badala ya kumeza vidonge kila siku bila shaka linafurahisha. Kukumbuka kumeza vidonge kila siku ni jambo linalohitaji umakini mkubwa,” amesema.

Anaamini wale wanaohitaji zaidi tiba mpya, kama vile wake wanaonyanyapaliwa zaidi, wanafaa kupewa kipaumbele kupewa tiba ya sindano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!