Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kishindo cha Magufuli saa 48 Dar
Habari za SiasaTangulizi

Kishindo cha Magufuli saa 48 Dar

Spread the love

 

JOHN Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, ameliteka Mkoa Dar es Salaam na viunga vyake, katika maeneo mbalimbali hususan, Uwanja wa Uhuru. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jana Jumamosi na leo Jumapili, ilikuwa ni fursa kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo jirani, kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Magufuli, aliyefariki dunia Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Tofauti na hali ilivyokuwa jana uwanjani hapo, leo umati mkubwa umejitokeza kutoa heshima za mwisho. Umati huo umeanza kufika uwanjani hapo toka saa 12 kasoro asubuhi.

Hadi jeneza lenye mwili wa Dk. Magufuli, linawasili majira ya saa 2 asubuhi, uwanja ulikuwa umejaa, huku nje kukiwa na wananchi wengi wakisubiri kuingia ndani.

Hata kabla ya shughuli ya kuanza kutoa heshima za mwisho kuanza, baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani na wengine nje, walionekana kudondoka kwa kuishiwa nguvu huku wengine wakipoteza fahamu.

Vikosi vya ulinzi na usalama ikiwemo Msalaba Mwekundu, walikuwa na wakati mgumu, kuwahudumia waombolezaji waliokuwa wakihitaji msada wa dharura kwani, walionekana kuzidiwa.

Magari ya wagonjwa, yalikuwa mengi kutoka hospitali mbalimbali, yakionekana yakitoka uwanjani hapo kuwapeleka hospitalini wale waliokuwa wakihitaji msaada zaidi.

Ukiwa kwenye viwanja hivyo, sauti za ving’ora vilikuwa vikisikika mara huku, mara kule huku Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gongwe, akionekana mara kwa mara kutoa miongozo na kuwatuliza wananchi waliokuwa wakipanga foleni kwenda kutoa heshima ya mwisho.

Mkazi wa Tabata, Andrew Msafiri anasema ‘’nimefika hapa tangu saa 12 asubuhi na mpaka sasa (ilikuwa saa 6 mchana), sioni hata dalili kama nitaweza kumuaga Rais wangu. Kama unavyoona, watu ni wengi sana.’’

Kutokana na umati huo kuwa mkubwa, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene alitoa maagizo ya waombolezaji waliokuwa nje ya uwanja, wafunguliwe mageti ya Uwanja wa Benjamin Mpaka.

Ni baada ya kule nje, kuwa wengi na kusababisha msongamano mkubwa ulioweza kuzua vurugu za kila mmoja kuingia ndani na walipoingia uwanja wa Mkapa, uliopo mkabala, nao ulijaa kwa majukwaa ya upande wa Uhuru.

Utofauti na jana ambapo waombolezaji walianza kuaga hadi saa 1 usiku, lakini leo imekuwa tofauti kwani, ilipofika mida ya saa 8 mchana, shughuli ilisimamishwa kwa muda.

Mkuu wa Wilaya Gondwe aliwatangazia waombolezaji, ‘’tunawaomba msubiri kwanza tuwaandalie utaratibu mwingine wa kuaga.’’

Utaratibu ambao ulianza kutumika ni tofauti na ule wa waombolezaji kuingia ndani ya kijumba maalum, lakini sasa utaratibu ulikuwa watu wanapita nje ya kijumba na kupunga mkono, kuonesha kumuaga mpendwa wao Dk. Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!