MAELFU ya wakati wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani, wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, katika Uwanja wa Uhuru. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Leo Jumapili tarehe 21 Machi 2021, ni siku ya pili na ya mwisho kwa wakazi wa Dar es Salaam, kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Magufuli kisha kesho Jumatatu, utaagwa kitaifa mkoani Dodoma ambapo ni siku ya mapumziko.
Idadi ni kubwa ya wananchi katika Uwanja wa Uhuru ambao wamejitokeza hali inayowapa wakati mgumu vyombo vya ulinzi na usalama kuweza kuwaongoza.
Majukwaa yamejaa huku umati mkubwa ukiwa bado nje ukisubiri kuingia.
Idadi ya wale wanaoishiwa nguvu nayo ni kubwa na huku gari za wagonjwa zipo za kutosha ambazo zimekuwa zikitoka kuwapeleka hospitali mbalimbali kwa huduma zaidi.
Dk. Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mfumo wa umeme.
Kutokana na idadi hiyo kuwa kubwa, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene aliagiza polisi kusimamia vyema watu kuingia na kutoka ili watu wote waweze kutoa heshima za mwisho.
Leave a comment