Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana: Naomba Rais Magufuli anisamehe
Habari za Siasa

Kinana: Naomba Rais Magufuli anisamehe

Spread the love

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amejitokeza hadharani na kumuomba msamaha Rais John Magufuli, kutokana na mazungumzo yaliyofanyika kwa simu kati yake na baadhi ya makada wa chama hicho, yaliyokuwa na nia ovu dhidi ya kiongozi huyo na chama chake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea)

Kinana anakuwa kada wa nne kumwomba radhi Rais Magufuli kutokana na mazungumzo hayo yaliyotikisa medani za siasa nchini mwaka 2019 kusambaa katika mitandao ya kijamii zikizungumzia kuporomoka kwa chama hicho na uenyekiti wa John Magufuli ndani ya CCM.

Mwanasiasa huyo mkongwe ameomba radhi kipindi ambacho yuko chini ya matazamio kwa miezi 18, kipindi ambacho hataruhusiwa kugombea uongozi wowote baada ya kamati kuu kutoa adhabu hiyo tarehe 28 Februari 2020.

Leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020, akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Kinana amesema amesema, wakati anashughulikia suala lake (ambalo hakulitaja) alitumia njia zisizokuwa sahihi.

“Najua nilikereka na vitu fulani na nikahuzunika na kukaairika katika kushughulika na suaa lile na kusema mambo ambayo hayakuwa mazuri kwa Rais na mwenyekiti wangu,” amesema Kinana

“Baada ya kutafakari nimeona niombe radhi kwa kusema ndugu mwenyekiti nimekukwaza, nimekuhuzunisha, nikuombe radhi kwa yale niliyoyasema,” amesema

Kinana amesema,”katika maisha ni uungwana kukaa na kutafakari na bila shaka atanisikia na atanisamehe.”

Kuhusu kuadhibiwa, Kinana amesema, suala la kuadhibiwa ni suala la kawaida pindi kiongozi au mwanachama anapojikwaa na wala yeye hatokuwa wa mwisho kuadhibiwa.

Wengine watatu waliosamehewa na Rais Magufuli baada ya kukwomba radhi na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM tarehe 13 Desemba 2019 kutoa msamaha ni wabunge wa chama hicho, William Ngeleja (Sengerema), Nape Nnauye (Mtama) na January Makamba (Bumbuli).

Nape yeye alikwenda Ikulu ya Dar es Salaam kumwomba radhi huku Januari na Ngeleja Rais Magufuli akieleza walimwomna ila haikuwa hadharani kama ilivyokuwa kwa Nape na sasa Kinana.

Makada wengine walioingia matatizoni kutokana na sauti hizo ni Katibu Mkuu mataafu wa chama hicho, Yusuf Makamba na Bernard Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje katika utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Wakati Kinana akipewa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 18, kamati kuu ilimsamehe Makamba huku Membe ikimfukuza uanachama kwa kile kilichoelezwa na CCM alikuwa na mienendo isiyoridhisha.

Membe anasubiri hatima yake kama mbele ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kuidhinisha kile kilichoazimiwa na kamati kuu cha kumfukuza au kumsamehe ndani ya chama hicho.

Kinana, Makamba na Membe walikutwa na kadhia hiyo baada ya kuwa wamehojiwa na kamati ya maadili iliyokuwa iliongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM- Bada, Philip Mangula.

Membe alihojiwa ofisi za CCM makao makuu Dodoma huku Kinana na Makamba mahojiano yao yakifanyikia ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Msingi wa mahojiano hayo ya sauti zao, yalitanguliwa na waraka wa Kinana na Makamba kuandika Julai 14 mwaka 2019 kwenda kwa Katibu wa Baraza la Wazee la CCM, Pius Msekwa wakidai uongozi hauwalindi dhidi ya mtu ambaye alikuwa akiwadhalilisha na walimwelezea analindwa na mtu mwenye mamlaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!