Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Bosi’ MSD, mwenzake kortini tuhuma za utakatishaji fedha
Habari Mchanganyiko

‘Bosi’ MSD, mwenzake kortini tuhuma za utakatishaji fedha

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itawafikisha mahakamani aliyekuwa mtendaji mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na mwenzake kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwemo utakatishaji fedha haramu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mwingine ni, kaimu mtendaji wa Lojistiki wa MSD, Gyekwaso Tabura kwa pamoja watafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.

Taarifa ya Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani aliyeitoa leo asubuhi Ijumaa tarehe 5 Juni 2020 amesema, wawili hao wanatuhumiwa kwa makosa ya kuisababishia serikali hasara, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na utakatishaji fedha haramu.

Wawili hao walishikiliwa na Takukuru tangu tarehe 2 Juni 2020 kwa mahojiano juu ya tuhuma hizo.

Bwanakunu alitiwa nguvuni ikiwa ni wiki chache kupita tangu Rais wa Tanzania, John Magufuli kutengua uteuzi wake wa bosi wa MSD tarehe 3 Mei 2020 kisha akamteua Brigedia Jenerali, Dk. Gabriel Mhidize kuchukua nafasi iliyoachwa na Bwanakunu.

Kabla ya uteuzi huo, Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!