December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Kitabu cha mahabusu chakutwa na kipisi cha pini

Spread the love

 

KITABUcha kumbukumbu ya mahabusu (DR) cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, kimeibua maswali baina ya shahidi wa Jamhuri na mawakili wa utetezi kwenye kesi ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hilo limejili leo Jumatatu, tarehe 22 Novemba 2021 wakati shahidi huyo, Ricardo Msemwa ambaye ni askari polisi, kituo cha Oyseterbay akitoa ushahidi wake, Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, mbele ya Jaji Joachim Tiganga. 

Kitabu hicho kimepokelewa kama kilelezo kikionesha watuhumiwa Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa walipokelewa na kufanyiwa mahojiano kituo hicho cha polisi huku watuhumiwa wenyewe wakikataa kufikishwa kituoni hapo.

Wakati shahidi huyo akiulizwa maswali na Wakili wa utetezi Peter Kibatala

amemuuliza maswali kuhusu kitabu hicho cha kumbukumbu ya mahabusu (DR)cha kukutwa na pini katikati.

Kibatala: Fungua DR ukurasa unaohusianana mshtakwia wa pili na wa tatu, hapo katikati kwenye kurasa kuna kinini?

Shahidi: Kwenye kinini?

Kibatala: (anamuone shashahidi) Umeoiona hii? Mwambie jaji, muoneshe aone katika kurasa inayomhusu mshtakiwa wa pili na wa tatu (Ling’wenya na Kasekwa)?

Shahidi: Hiyo ni stempla pini imedondokea

Kibatala: Chukua hiyo DR mwanzo hadi mwisho, tafuta nyingine yenye pini kama hiyo ukitoa kurasa inayohusu washtakiwa wengine iliyodondokea pini?

Shahidi anapekua

Kibatala: Tafuta kurasa nyingine yenye pini?

Shahidi: Hamna nyingine

Kibatala: Na wakati unatoa ushahidi wako ulifafanua uwepo wa hiyo pini kwenye kurasa?

Shahidi: Haikuwepo

Kibatala: Unasagest nani aliweka?

Shahidi: Sifahamu aliyeiweka

Kibatala: Lakini hukufafanua kama ilikuwepo au haikuwepo?

Shahidi: Haikuwpeo

Kibatala: Hukufafanua sababu haikuwepo?

Shahidi: Sikufafanua sababu haikuwepo

Naye Wakili wa Serikali, Pius Hilla alimtaka atoe ufafanuzi katika suala hilo akimuuliza, kuhusiana na pini kwenye kitabu na ukawa unajibu ya kwamba haikuwepo, ifafanulie mahakama haikuwepo wakati gani na kumekuwepo wakati gani?

Shahidi: Hii pin haikuwepo kuanzia wakati natoa ushaidi mara ya kwanza

Wakili Hilla: Uliulizwa swali ukasema hukufafanua na kwa kuwa pini ndiyo uliiona wewe, ieleze mahakama pini ya namna gani na inahusiano gani?

Shahidi: Hiki ni kipande cha nusu ya stempla kiko hapa lakini ipo katika ukurasa ambao Ling’wenya anaingizwa, kipo kati lakini kipo sehemu ya wazi. Nilisema sikufafanua sabahu haikuwepo. 

Shahidi huyo huyo amemaliza kutoa ushahidi wake leo na kesho Jumanne, ataendelea shahidi mwingine wa tatu.

error: Content is protected !!