MAWAKILI wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi imayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, wamepinga upokeaji wa nyaraka za upande wa utetezi, katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Andillah Ling’wenya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Mawakili hao wameweka pingamizi hilo leo Jumanne, tarehe 30 Novemba 2021, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.
Baada ya shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ndogo, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), mkoani Kilimankaro, Lembrus Mchome, jana kuiomba mahakama hiyo izipokee nyaraka hizo kwa ajili ya kielelezo.
Nyaraka hizo ni, barua ya Wakili Peter Kibatala, kwenda kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba mwenendo wa kesi iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo, nyaraka yenye taarifa za mwenendo wa kesi hiyo, dispach na hati ya mshtaka.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, uliweka pingamizi dhidi ya upokeaji nyaraka hizo ukidai shahidi anayetaka kuzitoa hana uwezo, pia nyaraka husika hazina umuhimu.
Wakili Kidando amedai wanapinga upokeaji wa nyaraka hizo kwa kuwa hazina umuhimu kwenye mwenendo wa kesi hiyo ndogo.
“Tuna mapingamizi kuhusiana na upokeaji wa nyaraka hizo zinazotaka kutolewa na shahidi wa pili. Tumegawa mapingamizi yetu kama ifuatavyo, pingamizi la kwanza kuhusu mwenendo wa kesi, charge sheet (hati ya mashtaka) pamoja na barua inayodaiwa kuandikwa kwenda kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, nyaraka hizi hazina relevance (umuhimu) katika proceeding zinazoendelea dhidi ya mshtakiwa wa tatu,” amedai Wakili Kidando.
Leave a comment