Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya kuvuliwa Ubunge: Lissu aiangusha Serikali
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya kuvuliwa Ubunge: Lissu aiangusha Serikali

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo tarehe 26 Agosti 2019, imetupilia mbali pingazi la Jamhuri kutaka kutosikilizwa ombi la Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mahakama hiyo mbele ya Jaji Sirilius Matupa, imamua kusikiliza maombo ya Lissu, yaliyowasilishwa na kaka yake Wakili Alute Mughwai, ambapo pamoja na mambo mengine, ameiomba mahakama itoe amri ya kuzuiwa kuapishwa kwa Miraji Mtaturu.

Jaji Matupa amesema, atasikiliza kesi hiyo kabla siku ya kuapishwa kwa Mtaturu (CCM) ambayo inaweza kuwa tarehe 2 Septemba ili kuzingatia haki za pande mbili, mbunge mteule na mbunge alivuliwa ubunge wake.

Kwenye uamuzi wake amesema, njia ya pekee ya kupinga kiapo ni kiapo kinzani na kwamba kwenye kiapo, ameziondoa aya zote zenye upungufu na kuziacha zenye mashiko.

Awali, upande wa Jamhuri uliweka pingamizi ukidai kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza shauri hilo, pia ulidai mwakilishi wa mpeleka maombi hana haki hiyo.

Mataturu (CCM) ni mbunge mteule aliyetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), baada ya tume hiyo kuendesha utaratibu wa kuziba nafasi aliyoiacha Lissu kufuatia uamuzi wa kuvuliwa ubunge.

Mteule huyo alitangazwa mshindi bila ya kupigiwa kura kwa kuwa ni pekee aliyerudisha fomu ya kuomba kugombea; waombaji wengine 12 wakitajwa kuwa hawakurudisha fomu zao.

Jimbo hilo lilikuwa wazi tangu tarehe 28 Juni 2019 baada ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kutoa tangazo la kumvua ubunge Lissu na kuiandikia NEC kwamba jimbo hilo lipo wazi.

Jaji Matupa ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 2 Septemba 2019, siku moja kabla ya Bunge la Jamhuri kuanza vikao vyako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!