April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kufufua shirika la uvuvi

Dk. Rashidi Tamatama, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Spread the love

SERIKALI imesema, iko mbioni kufufua Shirika la Uvuvi la Taifa (TAFICO), ambalo litawekeza katika uvuvi wa samaki kwenye ukanda wa bahari kuu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Rashidi Tamatama, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya uvuvi, ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Agosti 2019, wakati wa warsha ya uzinduzi wa kazi ya kupitia na kuandaa mpango mpya uvuvi.

Amesema, mipango ya serikali ya kulifufua TAFICO inatarajia kuwa na tija kubwa, kutokana na mipango iliyopo ya

serikali kufanya mchakato huo.

Na kwamba, mpango mpya wa uvuvi unaelekeza sekta kusimamia, kuhifadhi na kulinda ili sekta itoe mchango mkubwa kwenye lishe kwa mtu moja moja na usalama wa chakula.

Ester Mulyila, Kaimu Meneja Mkuu wa TAFICO amesema, shirika hilo lifufuliwa hivi karibuni katika menejimenti ya kufufua shirika hilo na kulifanyika utaratibu wa kuwateua watumishi.

Amesema, TAFICO ilianzishwa mwaka 1974, wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, ili kuendeleza shughuli za uvuvi, Makao Makuu yake yalikuwa Dar es salaam na lilifanya kazi Pwani yote ya Tanzania kuanzia Tanga, Mtwara, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

“Mpaka mwaka  2007 hapakuwa na mafanikio chanya ya ubinafsishaji wake, na serikali kupitia baraza la mawaziri ikatoa maelekezo  libinafsishwe tena kwa matumizi ya serikali.

“Kulikuwa na meli na mitambo mingi ambayo ilisimama kwa muda mrefu, kama meli na mitambo mingine. Mwaka 2008 Wizara ya Maliasili na Utalii iliyokuwa na dhamana ya uvuvi, iliuza vitu vinavyohamishika kwa taratibu za serikali na msajili wa hazina, lakini mali zisizohamishika – viwanja na majengo – vilibaki kwa matumizi ya serikali,” amesema.

error: Content is protected !!