HATIMA ya endapo Halima Mdee na wenzake 18 wataendelea kusalia kuwa wabunge itajulikana ndani ya siku 14 za usikilizaji wa shauri namba 27 la mwaka 2022. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Shauri hilo linalosikilizwa na Jaji Mustapha Ismail katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam limefunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya Bodi ya wadhamini ya Chadema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Halima na wenzake wanapinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho mara baada ya Baraza Kuu la chama hicho kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya kuwafukuza uanachama kwa makosa ya usaliti.
Leo Alhamisi tarehe 29 Juni, 2022, Mahakama hiyo imetoa kibali kwa wajibu maombi wote kuwasilisha viapo kinzani kesho Alhamisi tarehe 30 Juni, 2022 tayari kwa kuanza kusikiliza shauri hilo.
Hatua hiyo imejiri baada ya Kibatala kuiomba Mahakama hiyo kuondosha mapingamizi waliyowasilisha awali ili kupisha usikilizwaji wa shauri hilo kwa kuwa limefunguliwa mahakamani hapo kwa Hati ya dharura.
Jaji Mustapha Ismail amekubali ombi hilo na kuamua kuondoa mapingamizi hayo kabla ya shauri la msingi kuendelea kusikilizwa ambapo amesema kuwa amri ya zuio itaendelea mpaka shauri la msingi litakapofika mwisho.
“Baada ya kusikiliza hoja za Mawakili nimeamua Hati ya mapingamizi ya awali inaondolewa mapingamizi yote hayatataendelea”
Pia Jaji Mustapha amesema kuwa amri ya itaendelea mpaka mwisho wa shauri la msingi.
Leave a comment