Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Biashara Mbeya Kwanza zaaga Ligi Kuu
HabariMichezo

Biashara Mbeya Kwanza zaaga Ligi Kuu

Spread the love

 

Klabu ya soka ya Biashara United ya mkoani Mara rasmi imeshuka daraja na kuungana na Mbaya Kwanza iliyokua ishashuka daraja tayari baada ya Biashara kukubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Azam Fc leo 29 juni 2022 katika dimba la Azam Complex jijini Dar es salaam na hivyo kujikatia tiketi ya kucheza Championship msimu ujao. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco ….. (endelea)

Biashara ambao walikua na kiwango bora msimu uliopita na kumaliza kuafanikiwa kukamata nafasi ya nne kwenye msimamo na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa wanashuka daraja wakiwa wamekusanya pointi 28 katika michezo 30.

Timu hiyo inashika  nafasi ya pili kutoka mkiani hivyo kuungana na Mbeya kwanza ambaye leo kapata suluhu ya bila kufungana na Simba katika uwanja wa majimaji Songea hivyo watashuka moja kwa moja hadi Champioship ambapo Biashara wamekaa ligi kuu kwa zaidi ya miaka mitatu, Mbeya kwanza wao wamekaa msimu mmoja tu wamepanda na kushuka daraja

Aidha klabu ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons watacheza mechi ya play off ambapo mshindi ataenda kucheza na klabu ya JKT Tanzania ili kupata timu kukamilisha timu kumi na tano za msimu ujao na atakae poteza basi atakwenda Championship msimu ujao

Aidha klabu za Mbeya kwanza na Biashara United hazijashuka kinyonge kwani kila mmoja amejikulia kitita cha shilingi millioni kumi kutoka kwa wadhamini wa ligi na bonasi kutoka kwa Azam Tv , pia watapishana na Singinda Big stars pamoja na Ihefu Fc ambazo zimepanda msimu huu zikitokea Championship

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!