Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari Viongozi Zanzibar wafurahia ujio wa chuo cha CBE
Habari

Viongozi Zanzibar wafurahia ujio wa chuo cha CBE

Spread the love

 

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kinatarajia kujenga majengo ya Chuo hicho katika eneo la Fumba Zanzibar ambapo ujenzi wake utagharimu Sh. Bilioni 10. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea)

Ujenzi huo unatarajiwa kuanza kwa mwaka wa  fedha unaonza Julai mosi 2022/2023.

Uongozi wa chuo hicho ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo, Profesa Wineaster Suria Anderson, upo Zanzibar na umekutana na Uongozi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Wametembelea na kuoneshwa  eneo hilo la ardhi lilipo Fumba kwa ajili ya kukamilisha taratibu za umiliki wa eneo.

Akitoa wasilisho kwa niaba ya Uongozi wa Chuo  kikao hicho cha pamoja, Mkurugenzi Mipango wa Chuo hicho Dkt. Japhet Mtaturu, alisema kwamba wanahitaji kuongeza fursa za biashara Zanzibar na kutengeneza mazingira ya kuchochea ukuaji wa uchumi na taalamu kupitia elimu, tafiti na ushauri wa kitaalamu katika maeneo ya kibiashara.

Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema akifuatilia mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar ZIPA walipokwenda kwaajili ya kukabidhiwa eneo la kuwekeza

Alisema kutokana na kasi ya uchumi ni lazima kuwa na wataalamu wa biashara ambao watabobea na kuendeleza kasi hiyo na Zanzibar imejipanga kuwa na matukio bora ya kiuchumi hasa katika uchumi wa bluu na utalii.

“Sisi kama wataalamu tumejikita kuingia Zanzibar ili kuhakikisha tunaandaa watalamu watakaokuwa na maono makubwa na kasi iliyowekwa ya maendeleo kwa Zanzibar”alisema.

Alieleza kuwa kuazishwa kwa chuo hicho Zanzibar kuna tija katika tathimini ya kiuchumi na kitasaidia kuimarisha biashara za wajasiria mali.

Aliongeza kuwa  kuna watu wengi wamejiajiri katika sekta binafsi ambao wanafanya biashara mbalimbali lakini wanakwama kwa kukosa msaada wa kitaalamu hivyo kuazishwa chuo hicho kutasaidia kuinua sekta binafsi kwenye maeneeo ya wajasiriamali ili kukuza uchumi.

Profesa Eda Lwoga ambaye ni Naibu Mkuu wa Chuo, Mafunzo, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu CBE na na Emmanuel Munishi wakifuatilia mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar ZIPA walipokwenda kwaajili ya kukabidhiwa eneo la kujenga chuo huko Fumba Zanzibar

Mkurugenzi huyo alisema, pia chuo hicho kitachochea sekta ya utalii kupitia wageni kutoka Tanzania bara na nje ya nchi hasa ikizingatiwa kuwa chuo hicho kinaprogaram nzuri ya viwango na vipimo inayotolewa katika ukanda wa Afrika mashariki na kati na watu mbalimbali wanatoka nchi jirani kusoma katika chuo hicho.

“Kwa sababu Zanzibar ni mji ambao upo kitalii zaidi tunaamini kupitia program kama hizo tutatangaza utalii na kuinua uchumi wan chi.”alisema Dk Japhet.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Sharif Ali Sharif alifurahishwa na uamuzi wa chuo hicho kujenga tawi lake Zanzibar ambapo watawarahisisha wananchi kupata elimu ya biashara.

Aliushauri uongoozi wa chuo hicho kujitangaza zaidi ili kupata wananchi kutoka nje ya nchi ambao pia watafika Zanzibar baada ya kujenga majengo yao na kutoa huduma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sharif Ali Sharif akizungumza na viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), walipokwenda kukabidhiwa eneo la kujenga kampasi ya chuo hicho eneo la Fumba Zanzibar.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Profesa Wineaster Suria Anderson, alisema ni wakati mwafaka wa kuwa na tawi la chuo hicho Zanzibar kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma ya biashara na ujasiria mali.

“CBE kuingia Zanzibar kutakua na tija kubwa hasa katika biashara ikizingatiwa kuwa tunautaalamu wa kutosha wa kutibu changamoto zinazowakumba wajasiria mali katika biashara zao,”alisema.

Mwenyekiti huyo aliipongeza serikali ya Zannzibar kwa kukipatia chuo eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi huo kwa lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya elimu na biashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!