May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya kina Mbowe kusikilizwa kimtandao

Freeman Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa tarehe 13 Agosti 2021, inasikiliza kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu kwa njia ya mtandao ‘video conference.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake Halfani Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillahi Lingwenya watafuatilia kesi hiyo wakiwa katika mahabusu ya Gereza Kuu la Ukonga.

Tarehe 5 Agosti 2021, kesi hiyo iliposikilizwa kwa mtindo huo, haikufika mwisho na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo aliamua kuiahirisha kutokana na mtandao huo kuleta shida.

Mara baada ya kuiahirisha, ilipangwa tena kusikilizwa kesho yake yaani tarehe 6 Agosti 2021 na kutoa amri ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo wao wenyewe na si vinginevyo.

Leo Ijumaa, kesi hiyo ya uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi inayowakabili watuhumiwa hao, inatarajia kwamba, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) atawasilisha taarifa ya aina ya vielelezo na idadi ya mashahidi atakaowatumia kwenye kesi hiyo.

Ndani na nje viwanja vya mahakama ulinzi ni wa kawaida tofauti na ilivyokuwa tarehe 5 na 6 Agiosti 2021.

Getini hakuna prukushani zozote wanaofika wanaruhusiwa kuingia n ahata wafuasi wa Chadema hakukuwa na watu wengi nah ii inachangizwa na Mbowe mwenyewe kutokufikishwa mahakamani.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao ya kijamii kujua kinachoendelea mahajamani hapo

error: Content is protected !!