Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe waigeuzia kibao Serikali, Hakimu atoa agizo
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe waigeuzia kibao Serikali, Hakimu atoa agizo

Freeman Mbowe akiwa mahakamani
Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania-Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iwasilishe ombi lao Mahakama Kuu ya Tanzania la kupinga matamshi yaliyotolewa na Taasisi ya Serikali, dhidi ya mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi yanayowakabili mahakamani hapo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limewasilishwa mahakamani hapo leo Ijumaa, tarehe 13 Agosti 2021 na mawakili upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Akiwasilisha ombi hilo, Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala, amedai matamshi hayo ambayo hakuyataja, yataathiri mwenendo wa kesi hiyo.

Amedai, wateja wake wanayaona matamshi hayo kama hukumu, hivyo hawana imani kama mashtaka yao yataendeshwa kwa uhuru mahakamani.

“Tumeleta taarifa ya kusudio la kuiomba mahakama ipeleke Mahakama Kuu kama suala la kikatiba, matamshi yaliyotolewa na taasisi fulani hapa nchini, watu wote wanaifahamu, wamesikia.

“Tunachosema maneno yale au matamshi yale kwa maoni yetu sisi na wateja wetu, yameingilia uhuru wa mahakama. Sio mahakama hii tu, lakini mahakama itakayokwenda kusikiliza shauri la ugaidi linalowakabili washtakwia,” amedai Kibatala.

Katika maombi hayo, Mbowe na wenzake, wanaiomba Mahakama Kuu iangalie kama matamshi hayo yameingilia uhuru wa mahakama na kama itabainika yameingilia uhuru wa mhimili huo, kesi husika ifutwe.

“Kwa kuwa mamlaka ile yenye nguvu naishawishi basi matamshi yale kwa namna yalivyotamkwa, yamewafanya wateja wetu kuona tayari wamehukumiwa na kwamba hakuna namna yoyote wanaweza wakapata fair trial, tumeomba iangalie matamshi yale kama yameingilia uhuru wa mahakama,” amesema Kibatala.

Kibata ameongeza “na iwapo au la matamshi yale yamesababisha kesi isiwe na mantiki tena na hakuna la kufanya isipokuwa kufutwa.”

Kibatala amesema hayo nje ya Mahakama hiyo baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 27 Agosti 2021.

 

Awali, Wakili wa serikali Pius Hilla, alisema kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini washtakiwa wameshinmdwa kufikishwa mahakamani kutokana na kukosekana usafiri jambo lililopingwa na Kibatala, akisema walipaswa kuletwa mahakamani na si kama walivyofanya.

Mbowe na wenzake, walifuatilia kesi hiyo wakiwa Gereza Kuu la Ukonga kwa njia ya mtandao ‘video conference’ ambapo Hakimu Simba amewataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanawafikisha mahakamani hapo tarehe 27 Agosti 2021.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na wanahabari, alisema chama hicho kitachukua hatua za kisheria, kupinga kauli iliyotolewa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuhusu kesi ya Mbowe, akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Katika mahojiano hayo, Rais Samia aliwataka watu wanaoifuatilia kesi hiyo, kuiachia mahakama ionyeshe ulimwengu kama tuhuma za Mbowe na wenzake ni za kweli, au si za kweli.

Alipoulizwa kama Mbowe ameshtakiwa kwa makosa hayo kwa sababu za kisiasa, Rais Samia amejibu “mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa, kwa sababu ninavyojua Mbowe alifunguliwa kesi Septemba 2020, yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ya ugaidi na kuhujumu uchumi.”

“Nadhani wengine kesi zao zimesikilizwa, wengine wamepewa hukumu zao wanatumikia. Yeye upelelezi ulikuwa haujaisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea. Kwa hiyo amekwenda tumeingia kwenye uchaguzi,” alisema Amri Jeshi hiyo mkuu.

“Amemaliza uchaguzi, nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemhitaji waendele na kazi yao,” alisema Rais Samia.

1 Comment

  • Je, wakishindwa kumpeleka mahakamani maana yake hela nyingi zinatumika kuendesha kesi hii?
    Ni magereza au polisi?
    Anayejua atufunde.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!