May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kenyatta amwambia Samia ‘safari hii tutafika mbali’

Spread the love

 

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema, ana matumaini kwa taifa lake na Tanzania kufika mbali kutokana na kuimarika ushirikiano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Mei 2021, baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kenya. Rais Samia amefika nchini Kenya kwa zaira ya siku mbili (tarehe 4 – 5 Mei).

“…tunakuona kama dada yetu na nchi ya Tanzania na Kenya ni kitu kimoja, safari hiii tutaenda mbali sana kuhakiisha uhusiano wa nchi hizi unaendelea kuimarisha,” amesema Rais Kenyatta.

Akieleza mambo kadhaa aliyozungumza na Rais Samia, Rais Kenyatta amesema, wamekubaliana mambo mengi kwa lengo la kutimiza malengo ya waasisi wa mataifa haya mawili (Kenya na Tanzania).

“Tumezungumza kutahakikisha mambo ya biashara, uchumi, ya kitamaduni ambayo yamesaidia kujenga taifa letu la Kenya na Tanzania yanakuwa kwa manufaa yetu sisi wote.

“Tumekubaliana pia kuhusu masuala ya mawasiliano, namna ya kuimarisha safari za ndege, safari za reli, safari za baharini na safari za barabara,” amesema Rais Kenyatta.

Amesema, katika mazungumzo yao wamekubaliana kufanya haraka ya kuanzisha ujenzi wa barabara kutoka Malindi kuelekea Lungalunga mpaka kufika Bagamoyo.

“Tukasema, tutafurahia sana tukiona kuanzishwa safari zetu zile zilizokuwa kule Ziwa Victoria wakati wananchi na mzigo ilikuwa ikitembea kutoka upande wa Jinja kuja Kisumu kuelekea kule Mwanza na Bukoba,” amesema.

Kiongozi huyo wa Kenya amesema, amezungumza na Rais Samia kuhusu masuala ya usalama kwa nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na kukabiliana na vitendo vya kigaidi.

“Tumeweka mikataba kuhusu kujenga bomba la gesi kutoka Dar es Salaam mpaka Mombasa, na hiyo itarahisisha bei na kusaidia pia viwanda vyetu kupata nishati,” amesema na kwamba, suala la utalii ni miongoni mwa mambo waliyokubaliana na kiongozi wa Tanzania (Rais Samia).

Rais Kenyatta ameonesha furaha kukutana na Rais Samia kwa kuwa, ni safari ya kwanza kutembelewa na rais mama wa kwanza Afrika Mashariki kuwa rais.

“Tunakupongeza sana kwa nafasi uliyopatiwa kuongoza Tanzania pia tunakupongeza kwa uchaguzi wako hivi karibuni kuwa mwenyekiti wa chama tawala – CCM, tunakuhakikishia Kenya na serikali yangu itakuwa mstari wa mbele kushirikiana,” amesema.

error: Content is protected !!