Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Ndalichako aweka wazi vipaumbele 2021/22
Elimu

Prof. Ndalichako aweka wazi vipaumbele 2021/22

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako amebainisha vipaumbele vitakavyofanyiwa kazi mwaka wa fedha 2021/22, ikiwemo kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa lengo la kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Profesa Ndalichako, amebainisha vipaumbele hivyo, leo Jumanne, tarehe 4 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2021/21 ya Sh.1.38 trilioni.

Aidha, Profesa Ndalichako amesema, Serikali itafanya mapitio ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ili kuhakikisha inaendana na mazingira ya sasa ya utoaji wa elimu nchini.

Amesema, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali itaweka msisitizo zaidi katika ufundishaji wa masomo ya ufundi kwa kuimarisha mafunzo kwa vitendo katika shule za sekondari za ufundi.

Amezitaja shule hizo ni; Iyunga, Ifunda, Tanga, Bwiru Wavulana, Musoma, Mwadui, Moshi na Mtwara.

“Vilevile, Serikali itaimarisha ufundishaji wa masomo yanayowajengea wanafunzi ujuzi katika shule za msingi na sekondari.”

“Masomo hayo ni pamoja na Kilimo, ufundi, stadi za kazi, michezo, na biashara,” amesema Profesa Ndalichako.

Jambo jingine ambalo litatiliwa mkazo, Profesa Ndalichako amesema, Serikali itafanya ufuatiliaji na tathmini ya kina ya mitaala inayotumika kwa sasa ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji unafanyika kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.

“Vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa walimu kulingana na idadi ya wanafunzi, vitabu na mazingira ya kujifunzia.”

“Pia, Serikali itaanza kufanya mapitio ya mitaala katika ngazi zote za elimu ili kuhakikisha kuwa elimu na mafunzo yanayotolewa yanajikita katika kujenga ujuzi na kuzingatia mahitaji ya sasa,” amesema Profesa Ndalichako.

Waziri huyo amesema, mwaka 2021/22, Serikali itafanyia kazi maoni na ushauri wa wadau wa elimu kuhusu utekelezaji wa sheria ya mwaka 2018 iliyounda bodi ya kitaalamu ya walimu.

“Aidha, Serikali itazingatia pia maoni na ushauri wa kamati ya kudumu ya bunge ya sheria ndogo walioutoa katika majadiliano kuhusu kanuni za bodi ya kitaalamu ya walimu yaliyofanyika tarehe 28 Aprili 2021 kati ya Wizara ya Elimu na Kamati hiyo,” amesema Profesa Ndalichako.

1 Comment

  • Na yale maagizo ya JPM ya kufundisha somo la Historia kwa wanafunzi wote na madarasa yote yamefikia wapi? Yaani mabilioni yamepotea?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Spread the love  SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es...

error: Content is protected !!