March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Katibu wa Bunge aficha sababu za Ghasia kujiuzuru

Spread the love

HAWA Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini kupitia CCM, amejiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti leo tarehe 28 Agosti, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Vilevile, Jitu Soni, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo pia amejiuzulu wadhifa huo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Stephen Kagaigai, Katibu wa Bunge alipozungumza na mtandao huu kwa njia ya simu.

Hata hivyo, Kagaigai hakutaka kuzungumzia sababu zilizopelekea viongozi hao kujiuzulu zaidi ya kusema kwamba Bunge lina taarifa za kujiuzulu kwao.

MwanaHALISI Online ilimtafuta Hawa Ghasia kwa njia ya simu kwa ajili ya kutaka kupata ufafanuzi wa sababu za kujiuzulu kwake, hakupokea simu.

error: Content is protected !!