March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Channel za ndani kurudi kwenye ving’amuzi wiki ijayo

Spread the love

CHANELI za ndani kuanza kuoneshwa bure katika visimbuzi kuanzia tarehe 5 Septemba, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 28 Agosti, 2018 na Dk. Harrison Mwakyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maazimio yaliyotolewa katika kikao chake na wadau pamoja na wamiliki wa televisheni nchini.

Dk. Mwakyembe amesema kuanzia tarehe 5 Septemba mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Naye Dk. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

Kwa upande wa wamiliki wa televisheni, Dk. Abbasi amesema wameridhishwa na hatua hiyo.

error: Content is protected !!