Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kasi ya ukuaji NMB yawakosha wateja, waongezeka kwa asilimia 500
Habari Mchanganyiko

Kasi ya ukuaji NMB yawakosha wateja, waongezeka kwa asilimia 500

Spread the love

MBALI na huduma za viwango vya kifalme, wateja wa Benki ya NMB wamekiri kuvutiwa na mafanikio yake kiutendaji hasa kasi ya ukuaji wake ambayo wengi wamesema ni sababu ya wao kuendelea kuwa waaminifu kwa taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa kuzingatia hilo, wateja hao wamesema msimu huu wanasherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja duniani kwa kutambua pia mchango wa benki hiyo na huduma zake kwenye mafanikio yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye hafla ya maadhimisho hayo zilizondaliwa na benki hiyo kote nchini, wameishukuru benki hiyo kwa huduma bora na bunifu za kisasa.

Pia, wameipongeza kwa uimara wake na kusema kuenziwa na NMB imekuwa ni sehemu ya maisha yao na benki hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala (kushoto), mkuu wa idara ya Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Valence Mtongole (wapili Kulia) na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper wakifurahia kwa pamoja baada ya kupokea meza 100 na viti 100 kutoka kwa benki hiyo kwaajili ya shule za Sekondari za Samunge na Digodigo za wilayani Ngorongoro.

“Kwetu hii sherehe pia ni kwaajili ya kutambua mafanikio ya NMB, uwezo wake mkubwa kifedha na uimara iliyonao kiutendaji na kiuendeshaji,” alisema Shillah Mbogo, mwakilishi wa wateja wa tawi la Mlimani City.

Huko Babati mkoani Manyara, wateja wa NMB walisema benki hiyo inafanikiwa pia kwa sababu ya kuaminiwa na watu wengi kitu kinachoifanya kuongoza kwa idadi ya ambao sasa hivi ni zaidi ya milioni nne.

Kwa mujibu wa Aika Lema, vile vile NMB inawavutia wengi kutokana na uwekezaji wake endelevu kwenye miradi ya kijamii na ufadhili wa shughuli za jumuiya mbalimbali kama ilivyofanya siku kanda ya kaskazini kuadhimisha huduma kwa wateja.

Kupitia Mkuu wa Huduma Shirikishi, Valence Mtongole, NMB ilimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 22.

Afisa huyo alisema kwao Wiki ya Huduma kwa Wateja ni zaidi ya kuwaenzi watu wanaoifanya NMB kuwa benki kubwa kuliko zote nchini kwani pia ni nafasi ya kupata maoni kuhusu huduma zao na jinsi inavyoendeshwa.

“Mimi mrejesho wangu kwenu kama kiongozi na mteja ni kwamba NMB ni mdau mkubwa wa maendeleo wa mkoa wetu,” Makongoro alisema baada ya kupokea mchango wa mabati 600.

Lema ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Mati Super Brands Ltd., alisema NMB ni benki pendwa inayoweka maslahi ya wateja mbele lakini pia inayofuatiliwa kwa karibu sana.

“Inapopata faida tunajua, mapato yake yanaeleweka na mali zake zote ziko wazi Kiufupi, uwezi kukwama ukiwa mteja wa NMB kwa hiyo kuwa na msingi mpana wa wateja kwake ni rahisi,” alibainisha.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa wateja zaidi ya milioni nne iliyonao NMB sasa hivi ni ongezeko la zaidi ya asilimia 566 ya idadi ya iliyoanza nao biashara.

Pia inajivunia ukwasi wa zaidi ya Tsh trilioni 8 ukiliganisha na mizania yenye ukubwa wa bilioni kadhaa mwaka 1997 ilipoanzishwa.

Kuna wakati NMB ilikuwa na matawi 97 tu. Sasa hivi yamefikia 228 yakichochea kukua kwake na kujiimarisha sokoni ambako pia ina ATMs zaidi ya 800 na mawakala takribani 15,000.

“Nimekuwa mteja wa NMB tangu mwaka 2012 na tumekua pamoja. Nilipoanza kukopa nilipata TZS milioni 10 lakini sasa hivi nina sifa ya kukopa hadi TZS milioni 150,” alibainisha mteja mwingine wa NMB Babati, Bi Lydia Yahani Kasaini, ambaye ni Mkurugenzi wa Lemmy Enterprises.

Mikopo jumla ya NMB ilifikia TZS trilioni 4.8 mwaka jana hii ikiwa ni mara mbili zaidi ya ukopeshaji wa mwaka 2015. Aidha, NMB imekuwa inafanya vizuri kuhamasisha upatikanaji wa amana za wateja ambazo sasa hivi ni zaidi ya TZS trilioni 7.

Mwenyekiti wa Wajasiriamali wa Manyara, Ali Said Msuya, alisema yeye ni miongoni mwa wateja wanaovutiwa na jinsi NMB inavyotengeneza faida kubwa na kurudisha sehemu yake kwa jamii.

Kati ya mwaka 2015 na 2021, faida iliyopata NMB baada ya kodi iliyopaa kwa zaidi ya asilimia 93 kutoka TZS bilioni 150 hadi TZS bilioni 290.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!